1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Jamii ya kimataifa yalaani mauaji ya mwandishi habari wa Urusi

9 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD4c

Jamii ya kimataifa imeyalaani mauaji ya mwandishi habari wa Urusi, Anna Politkovskaya na imetoa mwito uchunguzi kamili ufanywe kikamilifu na kwa haraka.

Gazeti la Novaya Gazeta limeahidi kutoa yuro laki saba na nusu kwa mtu atakayetoa habari zitakazosaidia kumkamata aliyemuua mwandishi wake. Aidha gazeti hilo limesema litachapisha ripoti ya mateso yanayofanywa na wanajeshi wa Urusi huko Chechnya, ambayo Anna alikuwa akiitayarisha.

Polisi wanazuia komputya na vifaa nyengine vya mwandishi huyo vinavyohusiana na ripoti hiyo. Anna aliyekuwa akimkosoa vikali rais Vladamir Putin, aliuwawa juzi Jumamosi ndani ya jengo alikokuwa akiishi.

Umoja wa Ulaya na Marekani zimeyalaani mauaji ya mwandishi habari huyo, lakini mpaka sasa ikulu ya Kremlin ya Urusi bado haijasema lolote.