1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Moto mwingine wazuka katika hospitali.

10 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCkj

Kiasi watu wanane wameuwawa na wengine sita wamejeruhiwa katika moto uliotokea katika kliniki moja katika jimbo la Siberia, ikiwa ni tukio la pili la moto nchini Urusi katika hospitali kwa wiki hii.

Maafisa wamesema kuwa moto huo ulianza katika kliniki hiyo ya wagonjwa wenye matatizo ya akili katika mji wa Taiga katika jimbo la kusini la Kemerovo.

Tukio hilo linakuja baada ya tukio la moto ambao umetokea katika kliniki ya kuwalea watu wenye matatizo ya utumiaji wa madawa ya kulevywa mapema siku ya Jumamosi, ambapo watu 45 wanawake wameuwawa katika tukio ambalo linafikiriwa kuwa limeanzishwa kwa makusudi.