1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Rais Vladmir Putin aelekea Ujerumani kwa kikao cha G8

7 Juni 2007
https://p.dw.com/p/CBuD

Rais wa Russia, Vladmir Putin, ameelekea kwenye mkutano wa mataifa manane yaliyostawi kiviwanda, G8, huku akikabiliwa na shutuma za kimataifa.

Rais George W. Bush wa Marekani anatarajiwa kushauriana na Rais Vladmir Putin na amesema atamzungumzia kuhusu hali inayoendelea nchini Russia ya kukandamiza demokrasia.

Russia jana ilimtahadharisha Rais George Bush dhidi ya kutumia suala la demokrasia kama kisingizio cha kuingilia maswala ya ndani ya nchi hiyo.

Hali ya wasiwasi imeongezeka kati ya Russia na mataifa ya magharibi kutokana na mpango wa Marekani wa kujenga kituo cha kukinga makombora katika eneo la Ulaya Mashariki.

Hata hivyo Rais George Bush alisema kauli za hivi karibuni za rais wa Russia dhidi ya mataifa ya magharibi zimelengwa kwa wananchi wake hasa wakati huu ambapo uchaguzi mkuu umepangwa mwaka ujao nchini humo.