1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moscow. Russia haikubaliani na muswada dhidi ya Iran.

4 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwC

Russia imedai kufanyike mabadiliko makubwa kwa mapendekezo mengi ya bara la Ulaya kuiadhibu Iran kutokana na kukataa kwake kuachana na nia yake ya kujipatia teknolojia ya kinuklia.

China inaunga mkono msimamo wa Russia, na kuuita muswada huo uliotolewa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani kuwa unaiumiza sana Iran.

Marekani hata hivyo haifikiri kuwa muswada huo wa mataifa ya Ulaya unatoa adhabu ya kutosha kwa Iran.

Muswada huo utajadiliwa na wanachama kumi ambao si wanachama wa kudumu wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wiki ijayo.