1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW: Wagonjwa 45 wamefariki katika moto

9 Desemba 2006
https://p.dw.com/p/CCl5

Watu 45 wamefariki katika moto uliotokea Moscow nchini Urussi,kwenye hospitali inayowasaidia watu wanaotumia madawa ya kulevya,kurejea katika maisha ya kawaida bila ya madawa hayo.Isipokuwa kwa wawili,wahanga hao walikuwa wasichana waliokuwa watumiaji sugu wa madawa ya kulevya na walikuwa wakipokea matibabu katika hospitali hiyo.Maafisa wamesema,watu 10 wamejeruhiwa katika moto huo,baadhi yao wakiwa katika hali mbaya.Zaidi ya 100 wengine waliweza kutolewa nje ya jengo.Wahanga wote walikuwa katika wodi ya kike kwenye ghorofa ya pili ya jengo hilo lenye ghorofa tano.Kwa mujibu wa afisa wa zimamoto wa ngazi ya juu,moto huo ulianazishwa kwa makusudi.