1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MOSCOW:Raia ndio watakaomchagua mrithi wa Putin

1 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCW4

Rais Vladimir Putin wa Urussi amesisitiza kuwa mrithi wake atachaguliwa katika chaguzi za kidemokrasia.Alitamka hayo kwenye mkutano mkuu wa kila mwaka pamoja na waandishi wa habari mjini Moscow.Wakati huo huo lakini Putin akaongezea kuwa yeye atabakia na haki ya kumuunga mkono mgombea anaemtaka,wakati wa kufanywa kampeni za uchaguzi.Vile vile rais Putin anaeondoka madarakani mwezi wa Machi,alikanusha madai kuwa Urussi inatumia nguvu zake kama mzalishaji mkuu wa mafuta na gesi,kuendeleza malengo ya sera zake za kigeni.Katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita,Moscow mara mbili ilizuia kwa muda mfupi,usafirishaji wa gesi ili kuzishinikiza Ukraine na Belarus kukubali muongezeko mkubwa wa bei ya bidhaa hiyo.Kufuatia hatua hiyo,Umoja wa Ulaya umeuliza ikiwa Urussi inaweza kutegemewa kama muuzaji.