1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Moshi wa hatari mjini Moscow, Ujerumani yasaidia.

Abdu Said Mtullya8 Agosti 2010

Mabalozi wa nchi za kigeni waanza kuondoka Moscow.

https://p.dw.com/p/Oevj
Moto unaendelea kuwaka katika sehemu mbalimbali nchini Urusi.Picha: ap

MOSCOW:
Mabalozi kadhaa wa kigeni na wafanyakazi wa ubalozini wameanza kuondoka mjini Moscow pomoja na familia zao ili kuepuka moshi wa hatari unaoenea katika mji huo kutokana na sehemu mbalimbali kuendelea kuwaka moto.

Radio moja imearifu kwamba balozi za Poland, Austria na Canada tayari zimeshawarudisha nyumbani wafanyakazi na familia zao .

Wakati huo huo jumuiya ya kimataifa inaimarisha juhudi za kuisaidia Urusi katika kupambana na janga la moto.

Ufaransa inapeleka ndege zimamoto, na Italia pia imesema ipo tayari kupeleka ndege kadhaa za kuzimia moto.

Poland inapeleka wazimamoto 155 wakati Ujerumani imeitikia ombi la Urusi la kuipelekea nchi hiyo vitambaa maalum alfu mia moja vya kuzibia pua na midomo.

Ujerumani pia itapeleka mabomba ,pampu na majenereta.