1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mourinho kocha mpya wa Manchester United

28 Mei 2016

Manchester United imemtangaza rasmi Jose Mourinho kuwa kocha wake mpya akichukua nafasi ya Mholanzi Louis van Gaal aliyepewa mkono wa kwaheri

https://p.dw.com/p/1IwEw
England Chelsea Meister Jubel
Picha: Reuters/Sibley Livepic

Klabu hiyo imesema katika taarifa kwamba kocha huyo Mreno mwenye umri wa miaka 53 amemwaga wino kwa kusalia katika klabu hiyo kwa muda wa miaka mitatu na kuwa na uwezekano wa kuurefusha mkataba huo takriban hadi mwaka 2020.

"Kuwa kocha wa Manchester ni tuzo maalum katika mchezo huu," amesema Mourinho . " Ni klabu inayojulikana na kupendwa duniani kote. Kuna dhana na mapenzi kuhusiana na klabu hii ambavyo havipatikana katika vilabu vingine.

"Wakati wote nilijihisi kuwa na uhusiano na Old Trafford; kumekuwa na kumbukumbu muhimu kwangu katika wakati wote wa kazi yangu na nimefurahia uhusiano na mashabiki wa United. Mourinho ameendelea kusema. “Najisikia vizuri sana. Nafikiri fursa hii imekuja katika wakati sahihi katika muda wangu wa kufanyakazi kwasabanu Man United ni moja kati ya vile vilabu ambako unahitaji kuwa tayari kwasababu ni kile ninachoita vigogo, na klabu kigogo inapaswa kuwa na kocha bora kabisa na nafikiri niko tayari kwa hilo. Kwa hiyo naweza kusema ninajisikia raha, najisikia fahari, ni tuzo, ni kila kitu, lakini ukweli ni kwamba nanachopenda kufanya kazi na najisikia kuchelewa ninapongoja hadi Julai 7 kuingia uwanjani."

Mwandishi: Sekione Kitojo/AFP
Mhariri: Bruce Amani