1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mourinho kutumikia kifungo cha nje kwa ukwepaji kodi

Sylvia Mwehozi
5 Februari 2019

Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  kandanda ya  Real Madrid  na  Manchester United  Jose Mourinho  amepewa hukumu  ya  kifungo  cha  nje  cha  mwaka  mmoja  baada ya  kukubali  kuwa  ana  hatia  kwa  udanganyifu wa  kodi.

https://p.dw.com/p/3CkpX
Fußball Jose Mourinho Steuerhinterziehung Urteil
Picha: picture-alliance/dpa/Sputnik/N. Zotina

Kocha  wa  zamani  wa  klabu  ya  kandanda ya  Real Madrid  na  Manchester United  Jose Mourinho  amepewa hukumu  ya  kifungo  cha  nje  cha  mwaka  mmoja  baada ya  kukubali  kuwa  ana  hatia  kwa  udanganyifu  wa  kodi nchini  Uhispania siku ya Jumanne. 

Mourinho  hatatumikia  kifungo  jela  baada  ya  kukiri kufanya  udanganyifu  kwa  maafisa  wa  Uhispania  mwaka 2011 na  mwaka  2012. 

Hukumu  ya  miaka  miwili  ama  chini  ya  hapo  kwa  watu waliofanya  makosa  kwa  mara  ya  kwanza  inaweza kusitishwa  nchini  Uhispania. Mourinho  alifika  mbele  ya jaji katika  mahakama  mjini  Madrid  kuthibitisha makubaliano  ya  kukubali  kosa  aliyofikia  na  waendesha mashitaka. Kama  sehemu  ya  mpango  huo  pia atawajibika  kulipa  faini  ya  euro milioni  2.

Kocha  huyo  nyota  raia  wa  Ureno  mwenye  umri  wa miaka  56,  aliyefutwa   kazi hivi  karibuni  na  klabu  ya Manchester United  ya  Uingereza, alikuwa  kocha  pia  wa Real Madrid mwaka  2010  hadi  2013.