1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpambe wa Merkel apendekeza Brexit kupewa muda zaidi

John Juma Mhariri: Sekione Kitojo
17 Machi 2019

Mpambe mmoja wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuchelewesha tarehe ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kunaweza kutoa fursa ya Umoja wa Ulaya kutazama upya mkakati wake na namna ya kushauriana. 

https://p.dw.com/p/3FCE0
Deutschland CDU-Abgeordneter Detlef Seif im Bundestag
Picha: picture-alliance/dpa/Bildfunk/M. Kappeler

Suala la Brexit linatarajiwa kupewa kipaumbele katika mkutano wa viongozi wa Umoja wa Ulaya baadaye wiki hii. Tayari mpambe mmoja wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema kuwa kuchelewesha tarehe ya Uingereza kujitoa katika Umoja wa Ulaya kunaweza kutoa fursa ya Umoja wa Ulaya kutazama upya mkakati wake wa namna ya kushauriana na Uingereza. 

Uwezekano wa kurefusha tarehe ya mwisho ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya kutoka tarehe 29 Machi ambayo wabunge wa Uingereza walipigia kura kwa wingi, litakuwa ajenda kuu wakati viongozi wa Umoja wa Ulaya watakapokutana mjini Brussels wiki hii.

Japo Wajerumani ambao ni wahafidhina wangependa Uingereza isalie ndani ya Umoja huo la sivyo waziri mkuu Theresa May aridhie mpango uliokubaliwa kati ya pande hizo mbili, mwanasiasa wa kihafidhina wa Ujerumani Detlef Seif amesema kuwa ataunga mkono pendekezo la kuirefushia Uingereza tarehe ya kujitoa hadi mwisho wa mwaka 2020.

Na kwamba endapo tarehe hiyo itacheleweshwa, ameliambia shirika la habari la Reuters kuwa anapendekeza kuwa Umoja wa Ulaya ubadilishe miongozo au mikakati yake.

Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akilihutubia bunge lake 13.03.2019 kuhusu mpango wa Brexit.
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May akilihutubia bunge lake 13.03.2019 kuhusu mpango wa Brexit.Picha: picture-alliance/AP/M. Duffy

Uingereza ilipopiga kura ya kujiondoa Umoja wa Ulaya mnamo mwaka 2016, washauri wa Umoja wa Ulaya walishikilia muongozo wa hatua mbili, kukataa kujadili chochote kuhusu mustakabali wa mahusiano ya kibiashara, hadi pale Uingereza ilipotimiza masharti yake kifedha, ikakubali sheria rafiki kuhusu raia wa Umoja wa Ulaya ambao ni wataalamu, na kupata namna ya kuepuka mzozo wa mpaka kati ya Umoja wa Ulaya na jimbo la Uingereza la Ireland ya Kaskazini .

Lakini ugumu wa kuendeleza mashauriano kuhusu Brexit bila ya kuanza kuzungumzia masharti ya kibiashara katika siku zijazo, zimesababisha kuwepo matatizo kuhusu Umoja wa Ulaya kushikilia sera kuhusu mpaka ambao umewafanya wabunge wa Uingereza kukataa mpango uliokubaliwa.

Seif amesema kupiga hatua zaidi ya mfumo wa mashauriano unaotumika sasa, kutawaridhisha wafiasi wa Brexit katika bunge la Uingereza, likiwemo shirika la utafiti la Ulaya (ERG) linalohofia suala la mpaka wa Jamhuri ya Ireland na Ieland ya Kaskazini linaweza kuiacha Uingeza ikiwa imekwama ndani ya Umoja wa forodha wa Umoja wa Ulaya milele, kinyume na matakwa yake.

Seif ameongeza kuwa kisaikolojia, ni muhimu mfumo huo kubadilishwa kwa sababu shirika hilo la utafiti linafikiri kuwa hiyo ni njama.

Wanaharakati wanaounga mkono Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya wakiandamana nje ya bunge la Uingereza mnamo 27.02.2019
Wanaharakati wanaounga mkono Uingereza kujitoa Umoja wa Ulaya wakiandamana nje ya bunge la Uingereza mnamo 27.02.2019Picha: Getty Images/AFP/T. Akmen

Endapo tarehe ya Uingereza kujiondoa Umoja wa Ulaya yaani Brexit itacheleweshwa hadi mwisho wa mwaka 2020, basi viongozi wa Umoja wa Ulaya wanaweza kuwaagiza mafia wao kushauriana na Uingereza kuhusu mahusiano yao ya baadaye.

Sababu za msingi za kurefushwa kwa muda huo ni kujaribu kutatua misimamo mikali kuhusiana na suala la mpaka wa Jamhuri ya Ireland na Ireland ya kaskazini, huku akisisitiza kuwa pande zote mbili, Umoja wa Ulaya na Uingereza zitaweza kujieleza na kile wanachotaa kifanyike kuhusu suala hilo.

Seif anaamini kuwa wabunge wa kihafidhina wa Merkel katika bunge la chini huenda wakaunga mkono wazo hilo.

Kulingana na Seif, pendekezo lolote kutoka kwa Ujerumani ambaye ni mwanachama mwenye ushawishi mkuu wa Umoja wa Ulaya, kwamba umoja huo uachane na mfumo wake wa mashauriano na ufanye majadiliano yanayokubalika na Uingereza, huenda likakubaliwa haraka na wapinzani wa bibi May kama ishara ya uwezekano wa kuafikia mpango mzuri.

Kiongozi wa chama cha Angela Merkel alisema Ijumaa iliyopita kuwa Merkel anataka Uingerea ijitoe kstika Umoja wa Ulaya kwa utaratibu mzuri kwa hivyo Umoja wa Ulaya unapaswa kukubali kurefusa tarehe ya Uingereza kujiondoa.

Reuters