1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpango wa kufua uchumi Bungeni

14 Januari 2009

Kanzela Merkel Bungeni.

https://p.dw.com/p/GYNz
Angela Merkel na Frank-Walter Steinmeier .Picha: AP

Kanzela Angela Merkel wa Ujerumani kutoka chama cha CDU na hasimu yake katika kugombea wadhifa wa ukanzela katika uchaguzi wa baadae mwaka huu, waziri wa nje Frank-Walter Steinmeier (SPD) ambae taarifa za hivi punde zasema atarejea tena Mashariki ya kati, hawakupapurana hii leo Bungeni-Bundestag mjini Berlin wakati wa mjadala juu ya mpango wa serikali kuutia jeki uchumi:

Badala ya kuukaribisha mwaka huu wa uchaguzi mkuu kujipigia debe na kuvutia kura ,wanasiasa hawa wawili walikwepa changamoto ya aina hiyo.

Katika kikao maalumu bungeni mjini Berlin leo,Kanzela Angela Merkel na waziri wake wa nje Steinmeier, walijishughulisha na jinsi gani serikali itakabiliana na hali ya sasa ya kuzorota uchumi.Bw.Steinmeier alizungumza muda mfupi tu baada ya Kanzela Merkel kutoa tangazo la serikali kuhusu mradi huo wa Euro bilioni 50 wa kuufufua uchumi.

Risala ya wanasiasa hao 2 ililingana moja kwa moja: Kanzela Merkel alipendekeza kuimarisha nguvu zote na kuwanasihi wananchi kushikamana kwa m anufaa ya jamii nzima .waziri wa nje Steinmeier aliomba juhudi za pamoja za jamii nzima ili kuiokoa Ujerumani kutoka msukosuko wake mkubwa kudorora kwa uchumi tangu miaka 10 iliopita.

Mara moja waziri wa nje Steinmeier aliutupia machop uchaguzi ujao pale wakati wa mjadala Kiongozi wa chama cha Kiliberal FDP -upinzani,Guido Westerwelle alipomlenga yeye.Mwenyekiti wa FDP alisema mradi huo wa kuufufua uchumi usiowahi kupitishwa katika historia ya nchi hii baada ya vita vya pili hauridhishi kabisa.

Akijibu,Bw.Frank-walter Steinmeier,alimuonya mwenyekiti huyo wa FDP kwamba wakifanya mzaha hawataweza kujikomboa mwaka huu kutoka balaa hili la kiuchumi.

Akimgeukia kiongozi huyo wa FDP ambae kwa miaka mingi anadai kushirikishwa chama chake serikalini na binafsi kushika wadhifa wa uwaziri,Bw.Steinmeier alimwambia kwa ukali kuwa mwaka huu siasa hazitaki mchezo.Siasa zisiwe za porojo tupu.

Kanzela Merkel kwa upande wake alionya kati kati ya msukosuko huu wa uchumi hakuna anaetaka muakilishi ikiwa mwenyewe yupo kugombea uchaguzi.Alijaribu katika tangazo lake la serikali kuamsha imani ya wananchi kujiamini binafsi.

Alisema Kanzela Merkel kwamba msukosuko huu wa uchumi asilani hauhatarishi msingi wa uchumi wa Ujerumani,tangu kijamii hata kifedha. Uchumi wa Ujerumani unaendelea kuwa n a uwezo wa kushindana na unamudu kuvumilia dharuba zozote.

Kanzela Merkel akaongeza:

"Serikali za mikoa na za wilaya, zitapitisha hatua za kuufufua uchumi zisizowahi kuonekana katika historia ya Shirikisho la jamhuri ya Ujerumani".

Upinzani kwa upande wake haukonesha heshima yoyote katika mwito wa Kanzela na wa waziri wake wa mambo ya nje steinmeier:

Kiongozi wa kundi la wabunge wa chama cha Kijani cha mazingira, Fritz Kuhn aliikaripia serikali kwa kuwaokoa wanaviwanda kwa kuwachukulia dhamana ya mikopo minono.

Kwa kufanya hivyo, alikosoa, Kanzela Merkel amepotea njia.

Mwenyekiti wa FDP alisema kumtia waziri wa nje Steinmeier katika orodha ya leo ya wasemaji bungeni katika mjadala wa jinsi ya kufufua uchumi,kumeonesha nini hasa yajenda-nayo ni kampeni ya uchaguzi zaidi na sio mustakbala wa kiuchumi wa nchi hii.kitita cha Euro bilioni 50 cha kuutia jeki uchumi ni kama mfuko unaovuja.