1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mpendazoe aihama CCM

31 Machi 2010

Hatua hiyo si tone katika mto Rufiji

https://p.dw.com/p/MjS2

Joto la kisiasa linaonekana kupanda kila uchao nchini Tanzania, ikiwa imesalia miezi sita tu kabla ya uchaguzi mkuu. Hapo jana mbunge Fred Mpendazoe alijiengua kutoka katika chama tawala cha CCM na kujiunga na chama kipya ya Jamii, CCJ. kuna tetesi kwamba kuna vigogo wengine wanaokiunga mkono chama cha CCJ wanaopania kukihama chama tawala cha CCM.

Peter Moss amezungumza na Richard Kiaba, mwenyekiti wa Chama cha Jamii, CCJ kuhusu mabadiliko hayo katika mazingira ya siasa nchini Tanzania na kuanza kwa kumuuliza jinsi walivyoipokea hatua ya kujiunga kwa Fred Mpendazoe, Mbunge wa Kishapu, na chama chao cha CCJ.