1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mratibu mkuu wa misaada ya kiutu azuru Afrika

26 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CT36

Mratibu mkuu wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa, John Holmes, anatarajiwa kuwasili mjini Addis Ababa, Ethiopia hii leo kwa ziara ya siku mbili.

Akiwa nchini humo, John Holmes atakutana na maafisa wa serikali, Umoja wa Mataifa na wajumbe wa mashirika mengine yanayotoa misaada ya kiutu.

Atalitembelea pia eneo la Ogaden ambako atazungumza na wahanga wa mgogoro katika eneo hilo.

John Holmes anatarajiwa kwenda mjini Khartoum nchini Sudan keshokutwa Jumatano kabla kulitembelea jimbo la Darfur kuanzia Novemba 30 hadi Disemba mosi kukutana na watu waliolazimika kuyahama makazi yao.

Kiongozi huyo atamaliza ziara yake ya wiki moja barani Afrika mjini Nairobi, Kenya, kabla kurejea katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York.