1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mrengo wa Shoto Hamkani Ufaransa

24 Machi 2014

Chama cha siasa kali za mrengo wa kulia nchini Ufaransa FN kimezusha maajabu katika chaguzi za mabaraza ya miji zilizogeuka onyo kwa chama tawala cha kisoshialisti na kuwaruhusu wafuasi wa kihafidhina kusonga mbele.

https://p.dw.com/p/1BUmm
Mwenyekiti wa chama cha siasa kali za mrengo wa kulia Front National,Marine Le PenPicha: Reuters

Chama cha Front National kinachoongozwa na Marine Le Pen kimefaidika na ile hali kwamba idadi kubwa ya wapiga kura hawakuteremka vituoni, wakichoshwa na kashfa kadhaa zinazokigubika chama cha kihafidhina

Tukio jengine la kustaajabisha ni idadi ndogo ya wapiga kura walioteremka vituoni: asili mia 38.72 ya wapiga kura wameamua kutoteremka vituoni-

Mrengo wa shoto umepata pigo kubwa kupita kiasi katika wakati ambapo rais Francois Hollande amepoteza vibaya sana umashuhuri wake,miaka miwili tu baada ya kuingia madarakani .

Mijini Perpignan,Avignon,Forbach,Béziers,Fréjus,na Tarascon chama cha siasa kali za mrengo wa kulia FN kinaongoza matokeo ya duru ya kwanza.Na kina nafasi nzuri ya kushinda kwengineko pia baada ya ushindi wa moja kwa moja katika mji wa Hénin-Beaumont katika jimbo la kaskazini la Pas de Calais ambako Steeve Briois amekipatia ushindi chama hicho kwa mara ya kwanza katika mji wenye wakaazi zaidi ya elfu kumi.

Washoshialisti wajiweke matumaini Paris

Mjini Paris mgombea wa chama cha UMP Nathalie Kosciusko-Morizet anaongoza mbele ya mgombea wa chama cha kisoshiaalisti Anne Hidalgo.Hata hivyo mrithi wa meya aliyemaliza mhula wake Bertrand Delanoe anapewa nafasi nzur ya kushinda duru ya pili ya uchaguzi itakapoitishwa jumapili ijayo.

Frankreich Kommunalwahlen Paris Nathalie Kosciusko-Morizet und Anne Hidalgo Kombo
Wagombea wawili wa nafasi ya meya wa jiji la Paris(kushoto) Nathalie Kosciusko-Morizet wa chama cha kihafidhina cha UMP na (kulia) Anne HIdalgo Kombo wa chama cha kisoshialisti-.PSPicha: Joel Saget/AFP/Getty Images

"Hatukutarajia" amesifu M arine Le Pen aliyeutaja uchaguzi huo kuwa wa aina pekee na uliomaliza enzi za vyama viwili vya kisiasa.

Kwa mujibu wa matokeo ya muda yaliyotangazwa usiku wa manane wa kuamkia leo na waziri wa mambo ya ndani Manuel Valls,mrego wa kulia umejikingia asili mia 46,54,mrengo wa shoto asili mia 37.74,siasa kali za mrego wa kulia 4.65 na siasa kali za mrengo wa shoto asili mia0.58.

Serikali huenda ikabadilishwa

Wapiga kura milioni 45 wa Ufaransa na wale wa nchi za Umoja wa ulaya waliakiwa wakatoe sauti zao wakati wa uchaguzi huo ambao unaangaliwa kama kipimo cha umashuhuri wa rais Francois Hollande tangu alipochaguliwa mwezi Mai mwaka 2012.

EU Gipfel in Brüssel
Rais wa Ufaransa Francois HollandePicha: Georges Gobet/AFP/Getty Images

Rais Francois Hollande huenda akalifanyia mageuzi baraza la mawaziri."Hali inatisha" amesema msemaji wa serikali Nadjat Vallaud Belkacem.

Mwandishi:Hamidou Oummilkheir/AFP

Mhariri:Yusuf Saumu