1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mripuko wauwa mmoja na kujeruhi mwengine Paris

6 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYPG

PARIS

Bomu lililotegwa kwenye kifurushi limeripuka katika ofisi ya wakili katikati ya Paris leo hii na kumuuwa mtu mmoja na kumjeruhi mwengine vibaya sana.

Wizara ya mambo ya ndani imesema watu wengine kadhaa wamefadhaishwa na mripuko huo.

Jengo hilo lina ofisi ya taasisi yenye kufanya utafiti wa maangamizi ya Wayahudi na kampuni ya masuala ya sheria ambayo Nicolas Sarkozy ambaye hivi sasa ni Rais wa Ufaransa aliwahi kuifanyia kazi.