1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msaada wa Magna utagawanywa vipi?

15 Septemba 2009

Wawakilishi wa mataifa ya Ulaya na wa kiwanda cha kutengeza magari cha Opel wanapanga kukutana mjini Berlin hii leo kulijadili suala la kukigawa kiasi cha euro bilioni 4.5 kilizoahidiwa na serikali ya Ujerumani.

https://p.dw.com/p/JfIJ
Nembo za Magna na Opel

Wiki iliyopita serikali ya Ujerumani iliahidi kukipa kiwanda cha vipuri vya magari cha Magna msaada wa euro bilioni 4.5 utakaotumiwa kukiimarisha baada ya kukikinunua kitengo cha kutengeza magari cha Opel.Hapo jana kampuni ya Magna ilitangaza kuwa huenda ikazipunguza nafasi alfu 10,500 za kazi katika viwanda vyake kote barani Ulaya,nafasi 4,500 zikiwa Ujerumani pekee.

Chini ya makubaliano yaliyofikiwa mpaka sasa viwanda vyote vinne vya Opel vilivyoko hapa Ujerumani vinapaswa kuendelea na operesheni zake ila kuna tetesi kuwa kile kilichoko mjini Antwerp,Ubelgiji huenda kikafungwa.Ubelgiji na Uingereza zinaishawishi Kamisheni ya Umoja wa Ulaya kuhakikisha kuwa hatua hiyo ya kuiuzuia Magna kitengo cha Opel iwe na manufaa kwa mataifa yote husika badala ya kuyalinda maslahi ya Ujerumani pekee iliyoahidi msaada huo.

Mwandishi:Thelma mwadzaya /DPA