1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mshindi wa BoB atangazwa

7 Mei 2013

Mshindi wa blogu bora kabisa duniani anatarajiwa kujuilikana leo, baada ya jopo la majaji kwa kushirikiana na watumiaji kufanya maamuzi yao.

https://p.dw.com/p/18TQC
Chinese writer Li Chengpeng, looked upon by many as a a highly influential Chinese blogger and social commentator, attends a promotional event of his new book "SmILENCE" on January 26, 2013 in Kunming, southwest China's Yunnan province. Li was attacked by Maoists earlier at his book signings in Beijing and Shenzhen, forcing him to cancel two others in Guangzhou and Changsha. The Maoists take offence to Li's caustic essays and comments about the Communist Party?s governance. Li has previously been punched in the head at a previous signing. CHINA OUT AFP PHOTO (Photo credit should read STR/AFP/Getty Images)
Li ChengpengPicha: AFP/Getty Images

China, India na Misri zinashirikiana na Urusi, Uturuki na Ujerumani inaingia kwenye dakika za mwisho mwisho pamoja na Ukraine kwenye ukurasa huu. Hiki si kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa jijini New York, lakini maamuzi ya jopo la majaji wa Blogu Bora Kabisa jijini Berlin.

Wataalamu 15 wa mtandao wa Intaneti, wakiwemo wanaharakati, wanablogu na wanasayansi wanaamua nani ni washindi kwa kutumia vigezo sita. Baada ya mijadala ya wazi, sasa wanapaswa kuamua nani ni nani miongoni mwa maombi 4,200 kutoka duniani kote.

Blogu Bora Kabisa

Mwandishi wa Kichina, Li Chengpeng, ameshinda tuzo ya blog bora kabisa (kiungo: http://blog.sina.com.cn/lichengpeng). Nchini China, Li amekuwa mstari wa mbele kwenye vuguvugu la kupinga udhibiti wa serikali kwenye mitandao. Katika uzinduzi wa kitabu chake kipya, “Dunia nzima yajuwa” serikali ilimziba mdomo.

Li Chengpeng anaangaliwa na wengi kama mwanablogu mwenye nguvu sana nchini China.
Li Chengpeng anaangaliwa na wengi kama mwanablogu mwenye nguvu sana nchini China.Picha: STR/AFP/Getty Images

Katika “Kisomo cha kimyakimya,” Li Chenpeng anajitokeza akiwa na kizibo cha kupumulia na fulana iliyoandikwa “Ninawapendeni nyote.” Kizibo na fulana hiyo zimekuwa alama ya mapambano ya upinzani nchini China – vikiwa vimeigizwa mara milioni kadhaa. “Ni kigezo cha kuigwa na kizazi kipya. Anawashajiisha kujihusisha na kusimama dhidi ya udhibiti wa serikali kwenye mitandao,” anasema mjumbe wa jopo la majaji na mwanablogu, Hu Yong.

Kampeni Bora Kabisa Kwenye Mitandao ya Kijamii

Kampeni ya Vijana wa Morocco iitwayo Initiative 475 (kiungo: https://www.facebook.com/475LeFilm) iimechaguliwa kutokana na kujikita kwake kwenye haki za wanawake waliobakwa. Nchini Morocco, ikiwa mbakaji atamuoa aliyembaka, basi kwa mujibu wa Sheria Na. 475, mbakaji huyo hapewi adhabu.

Abdelouahab Errami, mmoja wa wanablogu wa Morocco.
Marokko BloggerPicha: Abdelmoula Boukhraiss

Hadithi ya Amina, ambaye alijiua mwaka 2012 akiwa na miaka 16, ni mada ya filamu “475” na kampeni ya kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Flickr. Mapambano hayo yalikuwa dhidi ya sheria hasa kutokana na mkasa wa karibuni wa ubakaji nchini India, “kampeni hii ni alama muhimu kwa wanaharakati kote ulimwenguni wanaopigania haki za wanawake,” lilisema jopo la majaji.

Ubunifu wa Hali ya Juu Kabisa

Lengo la huduma za blogu ndogo ya FreeWeibo.com (kiungo: https://freeweibo.com/) ni kuelezea tabia ya udhibiti wa mitandaoni ya serikali ya China. Jukwaa hilo hutoa fursa ya kutumia mtandao wa SinaWeibo.com bila kuchunguzwa na serikali, ambao ni moja ya mitandao mashuhuri kabisa ya kijamii.

Mtandao wa FreeWeibo wa China.
Webseiten der diesjährigen Bobsgewinner 2013Picha: freeweibo.com

Jopo la majaji linasema: “Udhibiti uliopangiliwa kimfumo ni moja ya matatizo makubwa kabisa nchini China kwa sasa. Ni baada tu ya kulifanya hilo kuonekana ndipo watu wanaweza kulibadilisha.”

Waandishi wa Habari Wasio Mipaka

Mwaka huu pia, kwa kushirikiana na Shirika la Waandishi wa Habari Wasio na Mipaka, BoB imeziangalia blogu ambazo zinafanya kazi ya kusifika kwenye suala la uhuru wa kujieleza. Tuzo maalum ya mwaka huu inakwensa kwa mwanablogu na mwanaharakti kijana wa haki za binaadamu, Fabbi Kouassi, kutoka Togo, Afrika ya Magharibi.

Blogu ya Fabbi Kouassi wa Togo.
Blogu ya Fabbi Kouassi wa Togo.Picha: fabbikouassi.wordpress.com

Anatumia blogu yake (kiungo: http://fabbikouassi.wordpress.com) kuripoti matumizi ya nguvu ya kupita kiasi yanayofanywa na polisi katika nchi hiyo yenye utawala wa kiimla. “Fabbi Kousassi anatetea uhuru kwenye nchi yake kwa namna ya kuvutia sana na hivyo kufanya jaala ya waandishi wa habari nchini Togo ijuilikane,” anasema Christian Mihr wa Waaandishi wa Habari Wasio na Mipaka juu ya uamuzi wa kumzawadia Fabbi Kousassi.

Tuzo ya Jukwaa la Vyombo vya Habari Ulimwenguni

Changamoto za kiuchumi duniani ndiyo maudhui ya mwaka huu ya Jukwaa la Deutsche Welle la Vyombo vya Habari Duniani (kiungo: http://www.dw.de/global-media-forum/home/s-30956) kuanzia tarehe 17 hadi 19 Juni. BoB imejikita kuangazia kigezo chake yenyewe, kwa kutilia mkazo kile kinachoitwa “Info Lady” kutoka Bangladesh.

Mradi wa Info Lady wa Bangladesh.
Infolady Projekt gewinnt Global Media Forum AuszeichnungPicha: D.net/Amirul Rajiv

“Info Ladies” ni wanawake wanaokwenda vijiji vya mbali visivyo na huduma ya Intaneti wakiwa na baiskeli zao. Wakiwa na kompyuta za mikononi na simu za kisasa, wanawasaidia wanavijiji hao kupata majibu kuhusiana na afya, kilimo na maendeleo. Kwa jopo la majaji “huu ni mradi wa kimapinduzi unaowapatia watu masikini wa Bangladesh taarifa muhimu.”

Tuzo ya Ubinifu wa Hali ya Juu na Halisi

Kipi tunachokiacha nyuma tunapotumia Intaneti? Hili ni swali ambalo linaangaziwa na mradi wa “Me and My Shadow” (kiungo: https://myshadow.org/). Mradi huu unawapatia watumiaji wa Intaneti kwa namna ya kuchekesha njia ya salama ya kuondoka kwenye mtandao wanaoutumia na kuwapa ushauri unaotekelezeka, kwa mfano, mabadiliko ya muundo wa ukurasa wa mtandao.

Me and My Shadow
Webseiten der diesjährigen Bobsgewinner 2013Picha: myshadow.org

Jumuiya ya kimataifa iitwayo Tactical Technology Collective ndiyo inayowapa mafunzo wanaharakati wa haki za binaadamu kushughulikia maendeleo mapya ya kiteknolojia duniani kote. Hasa kwenye nchi ambako kuna udhibiti na ufuatiliaji mkubwa wa serikali, hii ni hatua muhimu. “Baada ya yote, katika visa vingine huwa ni suala la kufa na kupona,” anasema mjumbe wa jopo la majaji Georgia Popplewell kutoka Trinidad na Tobago.

Tuzo ya “BoBs – Harakati Bora Kabisa Mtandaoni” ilianzishwa mwaka 2004 na Deutsche Welle kwa lengo la kushajiisha uhuru wa kujieleza kwenye mtandao wa Intaneti na kujenga jukwaa la mawasiliano lisilo udhibiti wa taasisi za serikali.

“BoBs ni jukwaa la kipekee, linaloonesha kuwa kuna tabia ile ile miongoni mwa watumiaji vijana wa mitandao duniani kote,” anasema mhariri mkuu wa DW, Ute Schaeffer. “Hatimaye kutakuwa hakuna namna yoyote kwa taasisi zenye nguvu kuichukua na kuifungia haki ya habari.2

Pamoja na jopo la majaji, watumiaji wa mitandao pia walikuwa sehemu ya maamuzi kwa kupiga kura ya blogu bora kabisa. Kwa majina ya washindi kwenye vipengele kadhaa, tembelea mtandao wa BoB, www.thebobs.com.

Mwandishi: Jan Bruck
Tafsiri: Mohammed Khelef
Mhariri: Mohamed Abdulrahman