1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msiwe na hofu! yasema EU kuhusu virusi vya H1N1

1 Mei 2009

Umoja wa Ulaya umepinga hatua ya kuzipiga marufuku safari za ndege zinazoelekea Mexico kitovu cha homa inayosababishwa na virusi vya H1N1 iliyopo kwa sasa.

https://p.dw.com/p/Hhsl
Nembo ya Umoja wa UlayaPicha: AP/DW

Kauli hiyo imetolewa baada ya Ufaransa kupendekeza hatua ya kupiga marufuku safari za ndege hizo kama njia moja ya kuzuia usambaaji wa virusi vya homa hiyo katika bara la Ulaya.Maafisa wa Afya wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Umoja wa Ulaya walikutana Luxembourg hapo jana ili kujadili mbinu za pamoja za kuzuia ueneaji wa virusi hivyo zinazojumuisha kushirikiana katika masuala ya dawa za kupambana na virusi hivyo pamoja na chanjo.

Grippevirus H5N1 soll für Vogelgrippe verantwortlich sein
Virusi vya H5N1 vinavyotokana na ndege chini ya mikroskopuPicha: DPA

Mkutano huo ulifanyika baada ya Shirika la Afya Ulimwenguni WHO kuongeza makali ya tahadhari ya kusambaa kwa virusi vya H1N1 hadi awamu ya tano.Hata hivyo bado halijakuwa janga la kimataifa.Virusi hivyo vimebainika katika mataifa 29 na mabara manne kote ulimwenguni.Canada imethibitisha kuwa mtu mmoja ameambukizwa virusi hivyo na binadamu.

Visa vipya vya maambukizi barani Ulaya vimeripotiwa Holland na Switzerland.Ujerumani,Uingereza,Uhispania na Austria kadhalika zimethibitisha kuwa virusi vya H1N1 vimeingia katika nchi zao nayo mataifa mengine ya bara hilo yako chonjo.

Mwandishi:Thelma Mwadzaya /RTRE,DPA,AFPE