1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msukosuko wa Hypo-Bank

5 Oktoba 2008

Kikao maalumu kimeanza wizara ya fedha Berlin kusaka ufumbuzi.

https://p.dw.com/p/FUQO
kanzla Angela Merkel na Rais wa Banki Kuu WeberPicha: AP

KIKAO KIMENZA KUIOKOA HYPO-BANK

BERLIN:

Wizara ya fedha ya Ujerumani, imetisha leo kikao cha dharura ili kusaka njia mpya ya kuiokoa Banki ya mikopo ya majumba - Hypo Real Estate -baada ya mpango wa Euro bilioni 35 kuporomoka hapo jana .

Banki hii ya Hypo Real Estate ni ya pili kwa ukubwa nchini Ujerumani ya utoaji mikopo.Ilisema jana mpango wa kuiokoa umeporomoka kwa kuwa wakopeshaji wa kibinafsi walirudi nyuma kusaidia.Mchango wa mabenki hayo ya kibinafsi ulikua muhimu katika mkakati mzima wa kuikoa benki hiyo.

Wakuu wanashauriana hivi sasa katika wizara ya fedha mjini Berlin ili kusaka suluhisho.Miongoni mwa wanaohudhuria kikao hicho ni Axel Weber, rais wa Banki Kuu ya Shirikisho ya Ujerumani,Josef Ackermann,mkuu wa Deutsche Bank-banki kubwa kabisa nchini Ujerumani.Baadae,Kanzela angela Merkel akitazamiwa kuzungumza na maripota juu ya ufumbuzi uliopatikana .