1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msukosuko wa Viwanda vya magari

29 Oktoba 2008

Mkutano unafanyika leo Brussels kuzingatia jinsi ya kuyaokoa makampuni ya magari ya Ulaya na msukosuko wa fedha.

https://p.dw.com/p/Fjnr

Kupunguka kwa masoko ya kuuza magari,viwanda vya magari kusimamisha uundaji magari,vilio kuvipatia msaada wa mabilioni viwanda vya magari,yote hayo yadhihirisha msukosuko ulioyakumba makampuni ya magari kutokana na athari za msukosuko wa fedha ulimwenguni. Umoja wa Ulaya lakini umejitolea kusaidia.Leo hii mjini Brussels,Ubelgiji wanashauriana wajumbe wa viwanda vya motokaa ,wale wa mashirika ya ulinzi wa mazingira na wa Tume ya Umoja wa Ulaya ,msaada huo uchukue sura gani.

Kampuni la motokaa la Daimler limetoa likizo ya lazima kwa watumishi wake wakati wa kipindi cha X-masi.Kampuni la BMW limepunguza uzalishaj viwandani nchini Ujerumani.Kampuni la FORD mjini Cologne, limeanzisha mtindo wa kufanya kazi nusu-siku.Kwa jumla, viwanda vya magari vimeingia kabisa katika msukosuko wa fedha.Na sio tu nchini Ujerumani, bali ulaya nzima.Kutimuliwa kwa umma wa wafanyikazi viwandani pengine hakutaepukika.

Mojawapo ya chanzo cha balaa hili ni hik asema Bw.Gunther verheugen,kamishna anaesimamia viwanda wa Umoja wa Ulaya kutoka Ujerumani:

"Nadhani chanzo chake ni wasi wasi uliozuka kutokana na mjadala wa kisiasa kuhusu mustakbala wa magari."

Motokaa isiochafua usafi wa mazingira ambayo haitapakazi i moshi mwingi, ni azma ya Umoja wa Ulaya katika mapendekezo yake ya ulinzi wa mazingira.

Verheugen aongeza:

"Hali hiyo imeongoza wanunuzi kujizuwia kwa sasa kununua magari na sababu nyengine bila shaka, ni msukosuko wa fedha ulioibuka na kuchangia zaidi katika wasi wasi huo. Ukiwepo wasi wasi juu ya hali ya uchumi siku zijazo,mtu huanza kuweka akiba na kubana matumizi ."

Lakini sio raia tu ambao wameingiwa na wasi wasi wakati huu.Kiwanda kizima cha magari kinaangalia usoni kwa jicho la wasi wasi.kwani, Umoja wa Ulaya mjini Brussels, unapanga kupitisha muongozo mkali kufuatwa na viwanda vya magari ili kulinda mazingira.Wanunuzi wa magari kwa sasa hawanuni , na viwanda vya magari vinapunguza utengenezaji magari.Hivyo unatoka balaa moja unaingia jengine.Vipi kukomesha hali hii, ndio shabaha ya mkutano wa leo wa kilele mjini Brussels unaohudhuriwa na vigogo vya viwanda vya magari.

Tayari uvumi umezagaa huko kuwa hatua za kwanza za kukabiliana na msukosuko huu kwa manufaa ya makampuni ya magari ya Ulaya zimeshaamuliwa au zitajadiliwa kwa upana na marefu. Makampuni ya motokaa yanapenda kutaja hali nchini marekani ambako mabilioni ya fedha yametolewa kama kiinua-mgongo kwa viwanda vyake vya motokaa .Hata viwanda vya magari barani ulaya, karibuni hivi vimepaza kilio hadharani kudai kupatiwa mikopo ya kiasi cha Euro bilioni 40.Fedha hizo ziwe raslimali katika taftishi na uundaji wa magari ambayo hayangetumia mafuta mengi.

Msaada wazi kutoka Brussels kwa viwanda hivyo vinavyopepesuka ,asema Bw.Gu nther Verheugen ,mjerumani kamishna anaehusika na viwanda wa UM ,yamkini ukatolewa.Lakini, anasema ule mpango wa kuyaokoa mabenki nchini Ujerumani hauwezi kuwa mfano wa kufuatwa naviwanda vya magari.