1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Msumbiji yatangaza hali ya dharura kufuatia wimbi la ghasia Afrika Kusini

23 Mei 2008

-

https://p.dw.com/p/E4si

JOHANNESBERG

Msumbiji imetangaza hali ya dharura huku serikali ikijizatiti kuwasaidia raia wake wanaoendelea kutoroka mashambulio ya chuki dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Msumbiji Oldemino Baloi hali ya dharura imetangazwa hii leo baada ya kiasi cha raia wake elfu 10 kukimbilia nchini kutoka Afrika Kusini.

Aidha amesema wimbi hilo la raia wake kurudi nyumbani litaongezeka kwasababu maelfu yao hawana pakwenda na wanaishi katika makaazi ya muda wakisubiri kusafirishwa msumbiji.

Ghasia dhidi ya wageni nchini Afrika Kusini zimeendelea kuenea kote ikiwa ni pamoja na mji wa Cape Town na maeneo ya mji wa Durban.Kiasi cha watu 42 wameuwawa na zaidi ya wageni elfu 25 wametoroka makwao tangu kuanza vurugu hizo mapema mwezi huu.