1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtandao wa ukahaba wavunjwa Uhispania

Sudi Mnette
5 Julai 2017

Polisi nchini Uhispania imeuvunja mtandao wa Ukahaba nchini Uhispania uliokuwa ukiendesha kazi zake haramu katika eneo moja la kitalii la mjini Puerto Banus

https://p.dw.com/p/2fzkE
Symbolbild policia
Nembo ya polisi ya UhispaniaPicha: picture alliance/dpa/J. Lizon

Jeshi limesema wanawake 13 walikuwa wamelazimisha kufanya kazi hiyo kwa shuruti katika eneo hilo vilevile wameachiwa huru. Duru zinasema inawezekana wanawake hao waliletwa katika eneo hilo kutokea Burgaria. Polisi katika pande zote mbili yaani Uhispania na Bulgaria wanasema wamewatia nguvuni watu wapatao 34, ambao walikuwa wakitoa vitisho kwa familia za waathirika endapo watakataa kufanya biashara hiyo ya ukahaba. Sio jitihada za muda mfupi kwa maana kwamba uchunguzi na jitihada nyingine zilianza kufanyika kwa takribani miaka mitatu iliyopita baada ya miongoni mwa wanawake hao kutoroka na kutoa siri. Pamoja na biashara hiyo wanawake wamekuwa wakitumika kuwafanyia vitendo vya wizi wateja na pia miongoni mwao wamo wanaotumia madawa ya kulevya.

Mwandishi: Sudi Mnette
Mhariri: Mohammed Khelef