1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtihani kwa chama cha AfD uchaguzi jimbo la Thuringia

Sekione Kitojo
27 Oktoba 2019

Uchaguzi utakaofanyika Jumapili katika jimbo dogo la mashariki mwa Ujerumani la Thuringia unaonekana kama mtihani mkubwa kwa uungwaji mkono wa chama cha kizalendo chama mbadala kwa Ujerumani, Alternative for Germany AfD

https://p.dw.com/p/3S0hS
Deutschland Bundesrat in Berlin | Bodo Ramelow (Die Linke), Ministerpräsident Thüringen
Picha: picture-alliance/dpa/S. Stache

Hali hii  inakuja  kufuatia  shambulio  la kigaidi  lililofanywa  na mfuasi  wa  siasa  kali  za  mrengo  wa  kulia mwezi  huu  dhidi  ya  sinagogi  tukio  ambao  lilizusha wimbi  la mshituko nchi  nzima.

Uungaji  mkono  wa  chama  cha  AfD katika  jimbo  la Thuringia kwa sasa  uko kati  ya  asilimia  20  na  24, kwa  mujibu wa  uchunguzi wa  hivi  karibuni wa  maoni  ya  wapiga  kura, hali  ambayo  inaweza kusababisha  chama  hicho  kinachopinga  wahamiaji  kuibuka  kuwa nguvu  ya  pili  kubwa  katika  bunge  la  jimbo  hilo.

AfD Björn Höcke l Wahlkampf-Veranstaltung der AfD  in Bad Langensalz, Thüringen
Mgombea wa chama cha AfD Björn HöckePicha: picture-alliance/dpa/M. Reichel

Wakati uungaji mkono wa  chama cha AfD umechupa  kutoka asilimia 10.6 katika  uchaguzi  wa  taifa  mwaka  2014, uungwaji wake  mkono  kwa  sasa  unaonekana  kuwa  chini  kwa  kile  chama hicho ilivyopata  katika  jimbo  hilo  mwezi  Agosti  na  Septemba.

Viongozi  wa  kisiasa  nchini  Ujerumani  wamejiunga  na  makundi ya  Wayahudi  katika  kulalamikia  shambulio  hilo  la  chuki  dhidi  ya wayahudi  hapo  Oktoba 9 katika  jimbo  jirani  la  Saxony-Anhalt kwa kiasi fullani  katika chama  hicho  cha  AfD.

Kamishna wa  serikali anayehusika  katika  mapambano  kupinga chuki dhidi  ya  Wayahudi  amekishutumu chama  cha  AfD wakati akiidhinisha  kile  kinachofahamika  kama "misimamo mingi ya kupiga chuki dhidi  ya  Wayahudi" wakati  wengine walikifananisha na  Wanazi mamboleo. Chama  cha  AfD binafsi  kimeshutumu shambulio hilo  la  risasi  kuwa  ni "uhalifu  mkubwa".

AfD Björn Höcke l Wahlkampf-Veranstaltung der AfD  in Bad Langensalz
Wananchi wakisikiliza hotuba ya kampeni ya mgombea wa chama cha AfD mjini Bad LangensalzPicha: DW/M. Strauß

Uchunguzi  wa  maoni  unaonesha  kuwa  waziri  mkuu  maarufu  wa Thuringia Bodo Ramelow anaweza  kupata  uungwaji  mkono  wa kutosha  kurejea  madarakani  baada  ya  kuwa  kiongozi  wa kwanza  mwaka  2014 kutoka  chama  cha  siasa  kali  za  mrengo wa  kushoto  cha  Die Linke  kuongoza serikali  ya  jimbo  nchini Ujerumani.

Lakini  kutokana  na  hali  ya  wasi  wasi  kabla  ya  uchaguzi kulikuwa  na  madai  kutoka  kwa  viongozi  wa  kisiasa  wa chama katika  jimbo  hilo, ikiwa  ni  pamoja  na  Mike Mohring, kiongozi wa chama  cha  kansela  Angela  Merkel cha  CDU  katika  jimbo  hilo kuwa  wamepokea  vitisho kutoka  kwa  watu  wenye  msimamo mikali  ya  mrengo  wa  kulia.