1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mtoto wa kiume wa Gaddafi na wajukuu 3 wauau

1 Mei 2011

Mtoto wa kiume wa mwisho wa kiongozi wa Libya Muammar Gaddafi, ameuawa katika shambulio la anga lililofanywa na jumuiya ya kujihami ya NATO.

https://p.dw.com/p/RLIt
In this photo taken Monday, Nov. 3, 2008, Libya's leader Moammar Gadhafi attends a wreath laying ceremony in the Belarus capital Minsk. Gadhafi's security forces unleashed the most deadly crackdown of any Arab country against the wave of protests sweeping the region, with reports Monday Feb. 22, 2011 that demonstrators were being fired at from helicopters and warplanes. After seven days of protests and deadly clashes in Libya's eastern cities, the eruption of turmoil in the capital, Tripoli, sharply escalated the challenge to Gadhafi. (AP Photo/Sergei Grits)
Rais wa Libya Muammar GaddafiPicha: AP

Msemaji wa serikali ya Libya, Mussa Ibrahim, akitangaza habari hiyo kwenye televisheni ya taifa amesema, Saif al-Arab, mtoto wa mwisho wa kiume wa Gaddafi ameuawa nyumbani kwake mjini Tripoli pamoja na wajukuu watatu wa Gaddafi.

Muammar Gaddafi na mke wake walikuwepo katika uwanja huo ulio na nyumba kadhaa, lakini wao wamenusurika. Saif al-Arab aliekuwa na miaka 29 ni mtoto wa kiume wa sita wa Gaddafi. Mussa Ibrahim amesema, shambulio hilo la anga limemlenga Muammar Gaddafi na limekiuka sheria za kimataifa. NATO bado haijatamka chochote kuhusu tangazo hilo wala haikuthibitisha.

Mapema hiyo jana, Gaddafi katika hotuba yake ya taifa alipendekeza kusitisha mapigano lakini vile vile alisema kuwa hatong'atuka madarakani wala hatoondoka Libya. Msemaji wa NATO Chris Riley amelipuuza pendekezo hilo kuwa "halina maana" na akasema mashambulio ya anga yataendelea ilimradi raia wa Libya wapo hatarini.