1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Muammar Gaddafi amefariki dunia

Martin,Prema/zpr/rtre21 Oktoba 2011

Waziri Mkuu wa Baraza la Mpito la Libya Mahmoud Jibril amethibitisha kifo cha kiongozi wa zamani Muammar al-Gaddafi.

https://p.dw.com/p/Rs5Z
Libya's National Transitional Council Prime Minister Mahmoud Jibril confirms the death of Moammar Gadhafi in Tripoli, Libya in this image taken from TV Thursday Oct. 20, 2011. Moammar Gadhafi, who ruled Libya with a dictatorial grip for 42 years until he was ousted by his own people in an uprising that turned into a bloody civil war, was killed Thursday when revolutionary forces overwhelmed his hometown, Sirte, the last major bastion of resistance two months after his regime fell. (Foto:APTN/AP/dapd) TV OUT
Waziri Mkuu wa Baraza la Mpito la Libya, Mahmoud Jibril akitangaza kifo cha Muammar GaddafiPicha: dapd

Akitangaza kifo hicho katika mji mkuu wa Libya Tripoli, Jibril amesema, wameungojea wakati huo wa kihistoria kwa muda mrefu. Sasa umewadia wakati wa kuwa na Libya mpya, Libya iliyoungana. Hapo awali, kamanda wa serikali mpya ya Libya alitangaza kuwa Gaddafi alijeruhiwa katika mapambano ya kuuteka mji wa Sirte, alikozaliwa kiongozi huyo wa zamani. Muda mfupi baadae alifariki kutokana na majeraha yake. Maiti yake imepelekwa katika msikiti mmoja mjini Misrata.

Libyan fighters celebrate in the streets of Sirte Libya in this image taken from TV Thursday Oct. 20, 2011. The Libyan fighters on Thursday overran the remaining positions of Moammar Gadhafi loyalists in his hometown of Sirte, ending the last major resistance by former regime supporters still holding out two months after the fall of the capital Tripoli. (Foto:APTN/AP/dapd) TV OUT
Wapiganaji wa Libya wakisherehekea mitaani Sirte, mji alikozaliwa Muammar GaddafiPicha: dapd

Inasemekana kuwa kiongozi huyo wa zamani wa Libya alikamatwa alipokuwa akikimbia kutoka mji wa Sirte katika mlolongo wa magari. Gaddafi anatazamiwa kuzikwa kwa siri baadae leo hii. Kwa mujibu wa ripoti za televisheni ya Libya, hata wanae wawili wa kiume, Saif al-Islam na Mutassim wameuawa. Maiti zao zimepelekwa hospitali mjini Sirte.

Mji huo wa pwani ulikuwa ngome ya mwisho ya Gaddafi na ulidhibitiwa na wafuasi wake mpaka dakika ya mwisho.Kifo cha kiongozi huyo wa zamani, kimeondoa kizingiti kilichokuwepo kwa serikali mpya ya mpito, miezi miwili baada ya waasi waliosaidiwa na nchi za magharibi kuuangusha utawala wa Gaddafi wa miaka 42 kwa kuuteka mji mkuu Tripoli.

USA Präsident Barack Obama Rede Sparplan
Rais wa Marekani Barack ObamaPicha: dapd

Nae Rais wa Marekani Barack Obama mjini Washington amesema, kifo cha Muammar Gaddafi kimefunga ukurasa mrefu wa maumivu kwa watu wa Libya. Akithibitisha kifo cha Gaddafi, Rais Obama alisema, hatimae utawala wa mabavu humalizika. Akasisitiza mchango uliotolewa na Walibya kumuangusha Muammar Gaddafi. Amesema, sasa watu wa Libya wenyewe, wanaweza kujiamulia mustakabali wa nchi yao.

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel amesema, hatimae njia ipo wazi kwa mchakato wa amani wa kisiasa. Wakati huo huo, Katibu Mkuu wa jumuiya ya kujihami NATO, Jemadari Anders Fogh Rasmussen amesema, sasa operesheni ya Libya itasitishwa kwani utawala wa Muammar Gaddafi umemalizika. Hata hivyo amesema, operesheni hiyo itasitishwa baada ya kushauriana na Umoja wa Mataifa na Baraza la Mpito la Libya.

epa02865596 Chairman of the Libyan National Transitional Council (TNC) Mustafa Abdel Jalil speaks during a press conference, in Benghazi, Libya, 13 August 2011. The TNC announced 08 august it had fired its executive board and asked Chairman Mahmoud Jibril to appoint a new one as part of the continuing fallout from the assassination of rebel General Abdul Fatah Younis. According to media reports, Rebel forces and Gaddafi soldiers are fighting at Gharyan a strategic city located about 50 kilometers from Tripoli. Reports also say that Libyan families try to flee the Libyan capital, as rebel pushing forward to Tripoli. EPA/STR +++(c) dpa - Bildfunk+++
Rais wa Baraza la Mpito, Mustafa Abdel JalilPicha: picture alliance/dpa

Shirika la habari la Ujerumani, DPA limewanukulu mabalozi wakisema kuwa Ijumaa ya leo, mabalozi wa nchi wanachama wa NATO watakuwa na mkutano wa dharura kuujadili mpango wa kumaliza operesheni za kijeshi nchini Libya. Lakini Waziri wa Mambo ya Nje wa Uingereza, William Hague mjini London, amesema, isifanywe haraka kuondoka na amekataa kupanga tarehe ya kuimaliza operesheni hiyo nchini Libya. Akaongezea kuwa operesheni hiyo ya NATO, itamalizika pale Baraza la Mpito la Libya litakapotaka.

Baadae leo hii, Rais wa serikali ya mpito ya Libya, Mustafa Abdel Jalil, anatazamiwa kutangaza rasmi kukombolewa kwa nchi hiyo kutoka utawala wa Gaddafi.