1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mudavadi amteua mgombea mwenza

22 Januari 2013

Mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya muungano wa Amani, Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi wa chama cha UDF amemteua mgombea mwenza kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa Machi 4.

https://p.dw.com/p/17OmH
Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi akiwa na Mkewe Tesse
Naibu Waziri Mkuu Musalia Mudavadi akiwa na Mkewe TessePicha: DW/J. Shimanyula

Hafla hiyo imefanyika katika makao makuu ya chama cha UDF mjini Nairobi siku moja baada ya vyama vya kisiasa kuwasilisha majina ya wagombea wao kwa tume ya uchaguzi nchini IEBC. Kura ya mchujo iliyokamilika mwishoni mwa wiki iliyopita ilikumbwa na vurugu huku ndugu wa Waziri Mkuu Raila Odinga wakijiondoa kwenye kinyang'anyiro cha Ugavana huko Kisumu na Siaya. Mwandishi wetu Alfred Kiti kutoka Nairobi na taarifa kamili.  Kusikiliza taarifa hiyo bonyeza alama ya spika za masikioni hapo chini.

Mwandishi: Alfred Kiti

Mhariri: Josephat Charo