1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Sinagogi mpya yafunguliwa Bavaria

9 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCuY

Sinagogi mpya ya Wayahudi imefunguliwa rasmi mjini Munich katika jimbo la Bavaria,kusini mwa Ujerumani.Sinagogi hiyo kuu imefunguliwa baada ya ile ya asili kuteketezwa na Wanazi takriban miaka 70 ya nyuma.Sinagogi na kituo cha jamii kitatumiwa na jumuiya ya Wayahudi wapatao 9,000 mjini Munich.Miongoni mwa wageni waliohudhuria sherehe hiyo ni rais wa Ujerumani Horst Köhler na balozi wa Israel Schimon Stein.