1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Syria na Iran zatuhumiwa kuchochea ghasia

27 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCXU

Waziri mkuu wa Lebanon,Fouad Siniora amezilaumu Syria na Iran kuwa zinachochea mapinduzi nchini Lebanon.Katika mahojiano yake na jarida la Kijerumani “Focus“ Siniora alisema,nchi hizo mbili zinawapa silaha wanamgambo wa Hezbollah na hivyo ghasia za upinzani zinahatarisha udemokrasia.Waziri mkuu Siniora anaeungwa mkono na nchi za magharibi amesema,Lebanon ni nchi ya Kiarabu inayotaka kubakia na udemokrasia.

KINSHASA:Katibu Mkuu Ban atembelea Kongo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Ban Ki Moon amewasili Kinshasa,nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo.Wakati wa ziara hiyo atakuwa na mazungumzo na rais Joseph Kabila na maafisa wengine pia.Katibu Mkuu Ban vile vile atavitembelea vikosi vya amani vya Umoja wa Mataifa vilivyokuwepo nchini Kongo.Tume ya Umoja wa Mataifa yenye kama wanajeshi 18,000 nchini Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo ni ujumbe mkubwa kabisa kote duniani.