1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

MUNICH: Ushirikiano na Urussi ni muhimu kutenzua migogoro

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTD

Mkutano wa usalama wa kimataifa ukiendelea katika mji wa Munich,kusini mwa Ujerumani,waziri wa ulinzi wa Marekani Robert Gates amesema, ushurikiano pamoja na Urussi ni muhimu katika jitahada za kutenzua migogoro duniani.Waziri Gates akiashiria tuhuma zilizotolewa na Rais Vladimir wa Putin wa Urussi amesema vita baridi vilivyokuwepo hapo zamani,vimetosha.Siku ya Jumamosi,Putin alipohotubia mkutano huo, aliituhumu serikali ya Marekani kuwa imesababisha usalama kupunguka duniani na imepuuza sheria za kimataifa.Vile vile akazionya Marekani na Shirika la Kujihami la nchi za Magharibi-NATO-dhidi ya kuwa na mitambo ya ulinzi ya kukinga makombora katika eneo la Ulaya ya Mashariki.Amesema,hatua hiyo itachochea urundikaji mpya wa silaha.Kwa upande mwingine Kansela Angela Merkel wa Ujerumani,ametoa wito wa kushirikiana kutenzua matatizo mbali mbali duniani.Leo hii,mkutano huo unajadili mgogoro unaohusika na mradi wa nyuklia wa Iran.