1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Museveni aongoza katika matokeo ya mwanzo

20 Februari 2011

Matokeo ya awali yaliyotolewa jana Jumamosi, yanaonyesha kuwa rais alie madarakani, Yoweri Museveni, anaongoza kwa takriban asilimia 71. Hiyo ni takriban mara tatu zaidi ya mpinzani wake, Kizza Besigye.

https://p.dw.com/p/R2W6
President Yoweri Museveni of Uganda addresses a press conference at Naklasero State House, Kampala, Thursday, Sept. 29, 2005. Museveni threatened Thursday to send troops within the next two months to neighboring Congo to disarm scores of Ugandan rebels there if U.N. peacekeepers and Congo failed to disarm them. (AP Photo/ Michael Makutu )
Rais wa Uganda, Yoweri MuseveniPicha: dpa

Hadi sasa kura milioni 5.5 ambazo ni sawa na asilimia 40 ambazo tayari zimeshahesabiwa. Hata hivyo, mgombea wa urais kwa tiketi ya IPC, Kizza Besigye ambaye ni mpinzani mkuu wa Rais Museveni ameilaumu Tume ya Uchaguzi ya Uganda kwa kukipendelea chama tawala cha NRM.

Präsidentschaftskandidat Kizza Besigye hält Rede aus offenem Auto Foto: Simone Schlindwein, 2.2.2011, Ibanda, Uganda
Mgombea urais Kizza BesigyePicha: DW

Kiasi ya wapiga kura milioni 14 kutoka jumla ya wananchi milioni 33 wa Uganda, walipiga kura Ijumaa iliyopita kumchagua rais wao ajaye pamoja na wabunge. Iwapo atachaguliwa tena, Rais Museveni anaetawala nchini humo tangu miaka 25, ataongeza utawala wake kwa miaka mingine mitano na hivyo kuungana na viongozi wengine wa Afrika, wanaotawala kwa zaidi ya miaka 30. Miongoni mwa viongozi hao ni Kanali Muammar Gaddafi wa Libya na Robert Mugabe wa Zimbabwe.

Wapinzani wa Rais Museveni walionya kuwa Uganda iko tayari kufuata mfumo wa maandamano yanayoendelea hivi sasa katika nchi za Kiarabu katika kudai haki zao, matamshi ambayo yalipuuzwa na Rais Museveni. Aidha, Tume ya Mawasiliano ya Uganda imeyaagiza mashirika ya simu kuzuia ujumbe mfupi wa maandishi wenye kutumia maneno "Tunisia", "Misri" na "Dikteta" ambayo yamo kwenye orodha ya maneno yanayoweza kuchochea vurugu.

Mwandishi: Grace Patricia Kabogo (AFP)

Mpitiaji: Martin, Prema