1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf akabiliwa na siasa nzito

Tuma Provian Dandi8 Oktoba 2007

Wakati Rais Perves Musharraf wa Pakistan akisherehekea ushindi wa kutetea wadhifa wake baada ya kuidhinishwa na Bunge, furaha yake imeingia nyongo kutokokana vifo vya wanajeshi wake wanne waliopata ajili ya helkopta

https://p.dw.com/p/C7iQ
Rais Perves Musharraf wa Pakistan
Rais Perves Musharraf wa PakistanPicha: AP

Furaha ya ushindi wa Rais Perves Musharraf ya kutetea nafasi kiti chake mwanzoni mwa wiki hii imegeuka kuwa simanzi baada ya wanajeshi wake wanne kupoteza maisha katika ajali ya helkopta, iliyotokea wakati wakienda katika mji wa Kashmir kwa kumbukumbu ya miaka miwili tangu kutokea tetemeko lililouwa watu wengi na kuharibu makazi ya watu milioni 3 na nusu.

Hata hivyo Rais Musharraf aliyepata kura nyingi katika uchaguzi wa bunge uliofanyika siku ya jumamosi hakupata madhara yoyote kutokana na kwamba alishafiri na helkopta nyingine katika msafara uliotangulia.

Msemaji wa jeshi la Pakistan Meja Jenerali Waheed Arshad amesema kati ya majeruhi wanane waliohusika katika ajali hiyo, yumo Meja Jenerali Rashid Qureshi ambaye ni msataafu.

Akikanusha ndege hiyo kuhujumiwa na kikundi chochote, msemaji huo amenukuriwa akisema kwamba ajali ya helkopta hiyo imetokana na matatizo ya kiufundi na kwamba hakuna dalili zozote kuwa imehujumiwa.

Lakini akasisitiza kwamba Rais Musharrafu alifika salama salimini na kwamba huko katika hali nzuri, isipokuwa ni maofisa wa kijeshi wanne pekee waliopoteza miasha.

Rais Musharraf ameshabahatika kuepuka majaribio matatu ya kuuwa na wanamgambo wanaosemekana kuwa na uhusiano na matandoa wa kimataifa wa Al Qaeda.

Tukio la mwisho aliloepuka mauaji ni lile lililotokea miezi mitatu iliyopita wakati akitoka kwenye kambi ya jesi ya Rawalpindi, ambapo hata hivyo shabaha ya washambuliaji iliikosa ndege yake wakati ikiondoka kwenye eneo hilo.

Awali Rais Musharraf aliahidi kuleta maridhiano nchini Pakistan atakapoanza ingwe mpya, japo kwa sasa anasubiri maamuzi ya Mahakama iwapo hatua ya kuidhinishwa na Bunge la nchi hiyo ni sahihi kisheria.

Hata hivyo kambi ya upinzani imezidi kumkosoa Rais Musharraf kutokana na mauaji mengi dhidi ya wanajeshi wa serikali pamoja na raia wa kawaida, huku pengo likizidi kuwa kubwa kati ya matajiri na maskini. Pia wanasema vitendo vya rushwa vimekuwa vingi zaidi.

Katika uchaguzi huo, Rais Musharraf alipata kura 252 kati ya 257 na ameshuruku kwa ushindi huo aliouita wa kidemokrasia, japo vyama vya upinzani viliususia.

Awali Rais Musharraf aliahidi kuachia ukuu wake wa majeshi ikiwa atashinda katika kinyang’anyiro hicho na kuwa rais wa kawaida kiraia.

Wakati uchaguzi huo ukifanyika wananchi wengi walikuwa na wasiwasi kuhusu maisha yao, ambapo baadhi wamepigwa na kujeruhiwa na askari wa kutuliza ghasia.