1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Musharraf kuondosha hali ya hatari Pakistan

10 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CZWD

Chama cha waziri mkuu wa zamani wa Pakistan,Nawaz Sharif kitashiriki katika uchaguzi wa bunge utakaofanywa tarehe 8 Januari nchini Pakistan. Chama cha Nawaz Sharif kilishindwa kumsadikisha mhasama Benazir Bhutto kususia uchaguzi huo, kupinga utawala wa hali ya hatari.Rais Pervez Musharraf alitangaza hali ya hatari tarehe 3 Novemba na hatimae aliwafukuza kazi mahakimu waliokuwa na maoni huru.Hatua hiyo ililaumiwa vikali sana ndani na nje ya Pakistan.

Lakini sasa kushiriki kwa vyama vingi katika uchaguzi ujao,kutatoa sura ya kufanywa uchaguzi ulio wazi na hivyo kuimarisha sifa ya Musharraf kuhusu demokrasia.Kwa upande mwingine,Rais Musharraf amearifu kuwa ataondosha hali ya hatari na kurejesha utawala wa kikatiba hapo tarehe 15 Desemba.