1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kali barani Afrika

Ramadhan Ali26 Septemba 2007

Mvua na mafuriko zimeathiri sehemu ,kubwa ya Afrika magharibi,afrika ya kati na hata Afrika mashariki.Uganda imeathirika mno huku thuluthi-moja ya ardhi yake iko chini ya maji.

https://p.dw.com/p/CHjC
Barabara iligeuka kuwa mto
Barabara iligeuka kuwa mtoPicha: AP

Tangu wiki kadhaa sasa, mvua kali zimekuwa zikinyesha na kusababisha mafuriko katika sehemu kubwa ya nchi za Afrika.Wachunguzi wanaamini kwamba, mvua hizi zimechangiwa pia na badiliko la hali ya hewa au uchafuzi wa mazingira.Hata mlinzi maarufu wa Uganda -mojawapo ya nchi zilizoathrika mno, Achilles Byaruhanga, anaona ‘mvua hizi “si za kawaida.”

Kuna hofu za kuzagaa kwa maradhi ya homa ya malaria,ukosefu wa chakula na ardhi ya kilimo na sio Uganda tu, bali kuanzia Gambia ,Afrika magharibi ,Afrika ya kati hadi Kenya na Ethiopia,Afrika Mashariki.

Hali bado haikupambazuka baada ya mwishoni mwa juma lililopita kwa mara ya kwanza baada ya muda mrefumvua ilisita kwa muda wa siku 3. Mvua hizi zilianza Julai,mwaka huu.Kwa jumla watu milioni 1.5 wmeathrika na maafa haya na Uganda pekee hadi watu laki 3 na hasa huko kaskazini na mashariki mwa Uganda.Hawana chakula ,wala maskani ,mashamba yao yamefurika maji na majumba yao yamejaa maji.Njia hazipitiki.Hofu ya kuzuka maradhi ya malaria imeongezeka.

Nchi Uganda watu nusu-milioni wameathiriwa na mvua hizi kali na mafuriko.Nchi nyengine mbali na Uganda zilizoathirika ni Mali ambako watu hadi 41,000 wanahitaji msaada.

Burkina Faso watu 160,000,Sudan laki 6 na 25,000.Jirani yake Ethiopia hadi watu 226,000 wamedhuriwa na mafuriko .

Je,misaada kutoka mashirika ya kimataifa inawafikia watu hawa ? Vipi watu mfano huko kaskazini na mashariki mwa Uganda wanasaidia ?

Kwa mkereketwa wa mazingira nchini Uganda, Achilles Byaruhanga,mvua hizi ni ushahidi kuwa hali ya hewa imebadilika na ndio iliopelekea balaa hili.Byaruhanga alinukuliwa kusema,

“Wakati ninazungumza nawe hapa, thuluthi-moja ya Uganda iko chini ya maji.Watabiri wa hali ya hewa katika nchi jirani ya Kenya ,wamethibitisha kwamba kila kukicha wanajionea mabadiliko ya tabia ya hali ya hewa barani Afrika.Peter Ambenje,asema ukilinganisha jinsi mvua zilivyokuwa zikinyesha mnamo miaka 25 iliopita na hali ilivyo sasa, utaona ukame na mafuriko umeongezeka mno.

Ripoti iliochapishwa mwanzoni mwa mwaka huu juu ya hali ya hewa barani Afrika ya shirika la IPCC) imebashiri mbali na kuongezeka kwa ujoto wa wastani,kumeongezeka pia kwa mvua na ukame.

Mvua hizi zimeathiri nchi zaidi kama Kamerun,Nigeria,Sierra leone,Liberia,togo hadi Ivory Coast.

Kutokana na mmonyoko wa ardhi,mashamba yenye rutba yanatoweka.Kuna jamaa walioshindwa hata kuzika maiti zao,kwani kule kwenye makaburi kumesheheni maji.

Chini ya hali hii, hofu za kuzagaa kwa mbu na hivyo maradhi ya malaria zimeongezeka.Watu hawakujiandaa kujikinga na mafuriko,kwavile kamwe hawakuyatazamia. Iliosalia ni kutumai kwamba ,baada ya dhiki si dhiki,bali faraji.