1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvua kali zasababisha mafuriko Zimbabwe

21 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CehE

HARARE:

Watu wasiopungua 9 wakufa maji nchini Zimbabwe kufuatia mvua kali ambayo imekuwa ikinyesha kwa siku nchini humo.Taarifa kutoka Zimbabwe zinasema kuwa mvua hizo zimesababisha mafuriko katika maeneo kadhaa nchini humo.Gazeti linalomilikiwa na serikali la Herald linasema wengi wa waliopoteza maisha yao wanapatikana katika wilaya za nyanda za chini katika mkoa wa kusini wa Masvingo,ambako walizama katika mito ilokuwa imefurika maji.

Kwa mujibu wa idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Zimbabwe,mvua kali zitaendelea kunyesha katika sehemu kadhaa nchini humo.