1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano kati ya Kenyatta na Ruto unamaanisha nini?

11 Januari 2021

Nchini Kenya migawanyiko ya kisiasa inaendelea kupamba moto hasa baina ya rais Uhuru Kenyatta na makamu wake William Ruto. Wiki iliyopita rais Kenyatta alisema Kenya sio nchi inayostahili kuongozwa na makabila mawili tu, yaani Wakikuyu na Wakalenjin. Kauli hiyo ilitafsiriwa kuwa dongo kwa makamu wake Ruto na kambi yake. Saumu Mwasimba amezungumza na Professa Chacha Nyaigoti kuchambua mvutano huo.

https://p.dw.com/p/3nmIh