1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mvutano katika chama cha Rais Kibaki wa Kenya, PNU

25 Julai 2008

Nchini Kenya chama cha Rais Mwai Kibaki cha PNU kinakabiliwa na mivutano ya ndani kufuatia pendekezo lake la kuvunjwa vyama binafsi wanachama wa muungano huo.

https://p.dw.com/p/Ejju
Rais Mwai Kibaki wa KenyaPicha: AP Photo

Chama cha PNU kina vyama vitano wanachama kikiwemo KANU,Narc-Kenya,Safina,Ford-Kenya na Sisi kwa Sisi.Kwa mujibu wa mswada uliopitishwa bungeni hivi karibuni vyama vyote vya kisiasa nchini vinapaswa kuhakikisha kwamba hakuna mwanasiasa au mbunge anajiunga na zaidi ya chama kimoja cha siasa.Vyama hivyo vimepewa muda wa mwezi mmoja kutimiza hilo.

Kutoka Nairobi Mwandishi wetu Mwai Gikonyo anaarifu zaidi.