1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwafaka haujafikiwa Kenya lakini ipo dalili ya matumaini?

9 Februari 2008

Katibu mkuu wa zamani wa UN asema wiki ijayo wanaweza kupata ufumbuzi

https://p.dw.com/p/D4p8

NAIROBI

Serikali ya Kenya imeondoa amri ya kukataza mikutano ya hadhara ikiwa ni karibu miezi miwili baada ya uchaguzi uliogubikwa na utata ambao ulizusha ghasia kote nchini humo kufuatia kutangazwa rais Kibaki kuwa mshindi wa uchaguzi huo.

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa bwana Kofi Annan ambaye anaongoza mazungumzo ya kutafuta suluhu katika mzozo wa kisiasa kati ya serikali na upinzani nchini Kenya amesema hatua muhimu imepigwa kwenye mazungumzo ya jana ambapo amesema pande mbili zinafikiria uwezekano wa kuunda serikali ya pamoja na kwamba kunahitajika suluhisho la kisiasa.

Zaidi ya watu 1000 waliuwawa katika ghasia za uchaguzi na wengine laki tatu na nusu wakaachwa bila makazi tangu alipotangazwa mshindi rais Kibaki katika kile upinzani unachosema ni matokeo yaliyopikwa.Wasimamizi wa kimataifa kwenye uchaguzi huo wa Kenya pia walisema mizengwe ilifanyika.