1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka mmoja baada ya akina baba kuanza kulipwa ,mama anapojifungua

Hamidou, Oumilkher30 Oktoba 2008

Jee ni mapinduzi ya kweli au yale yale ya zamani,wanajiuliza wahariri

https://p.dw.com/p/FkLN
Waziri wa familia wa serikali kuu ya Ujerumani bibi Ursula von der LeyenPicha: picture-alliance/dpa




Mada kuu magazetini hii leo ni pamoja na  hali ya mambo namna ilivyo mashariki ya jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo na malipo ya wazee baada ya mtoto kuzaliwa nchini Ujerumani .


Tuanzie Ujerumani,ambako waziri wa familia Ursula von der Leyen anasifu ufanisi wa mpango wa malipo ya wazee baada ya mama kujifungua,mwaka mmoja baada ya mpango huo kuanza akufanya kazi.Gazeti la Die Welt linaandika:


"Malipo ya wazee ni jambo la kushangiriwa:Furaha iliyoje.Kuanzishwa  huduma hizi za jamii ni sawa na mapinduzi" anajisifu bibi Ursula von der Leyen.Lakini hata SPD na CSU wanasifu mageuzi hayo ya maana yaliyotiwa njiani na serikali kuu ya muungano mjini Berlin.Habari za kutia moyo zimegeuka tunu siku hizi.Hata hivyo turuhusiwe kuuliza ;Eti kweli ufanisi ni mkubwa hivyo kama unavyopigiwa upatu?Kiwango chenyewe cha malipo ya wazee si cha kushangiria:Idadi ya watoto waliozaliwa si kubwa hivyo ikilinganaishwa na mwaka mmoja kabla ya hapo,mtoto mmoja na nukta 37 kwa kila mama.Kwa hivyo Ujerumani inasalia kua nchi ambayo matumaini ya kupata watoto hayakukamilishwa."


Hayo ni maoni ya Die Welt,nalo gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linaandika:


"Kwa mtazamo wa kijuu juu mtu anaweza kusema malipo ya wazee,ndio yenyewe.Lakini ukiangalia kwa undani zaidi utagundua kwamba,yale mapinduzi ambayo  waziri von der Leyen anayapigia upatu,si chochote chengine isipokua yale yale ya zamani.Mpaka leo bado kiwango cha fedha anazolipwa baba akiamua kukaa nyumbani kulea mtoto ni haba.Wengi wao hawasalii zaidi ya miezi miwili nyumbani-muda ambao ni sawa na likizo iliyorefushwa tuu.Na ukimulika hali ya mambo katika ghorofa za juu wanakoketi wakubwa wakubwa ,hakuna dalili ya kubadilika hali ya mambo.Lingekua jambo la maana kama wao wakubwa kwanza wangeonyesha mfano mzuri wa kuigizwa ili kuwaondolewa hofu na wasi wasi wa kufukuzwa kazini au kufanyiwa tashtiti wafanyakazi wenzao wa kiume."


Na kuhusu hali katika jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo,gazeti la WESTDEUTSCHE ALLGEMEINE ZEITUNG,linasema"Kwa mara nyengine tena watu wanalazimika kuingia njiani kusalimisha maisha yao"Gazeti linaendelea kuandika:


"Kwa mara nyengine tena waasi wanapiga doria majiani,nyumba zinavunjwa na wanawake kunajisiwa.Kwa mara nyengine tena vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa mataifa vinajikuta kati kati ya mapigano.Amani au kama waasi watavuliwa silaha na tume ya Umoja wa mataifa,hakuna hata mmoja anaeamini katika eneo la mashariki la jamhuri ya kidemokrasi ya Kongo."