1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka tangu Kosovo kutangaza uhuru

17 Februari 2009

Kosovo yasherehekea uhuru wake leo bila ridhaa ya Serbia.

https://p.dw.com/p/GwA2
Bendera ya Koso huruPicha: AP

Mkoa wa zamani waq Yugoslavia wa Kosovo unaokaliwa na waalbania wengi,unaadhimisha hii leo mwaka tangu kujitangazia uhuru na hii licha ya onyo la Rais Fatmir Sejdu kuwa Serbia ingali inalipinga tangazo hilo la uhuru.

Ramadhan ali na ripoti zaidi:

Kosovo ndio mkoa wa mwisho wa Shirikisho lililosambaratika la Yugoslavia kujipatia uhuru wake.

Waziri mkuu wake Hashim Thaci akitoa tangazo hilo la uhuru siku kama leo mwaka uliopita alisema:

Sisi Wanaume na wanawake tuliojitoa mhanga kwa ajili ya kosovo,tunanadi tukiwa waakilishi waliochaguliwa wa umma kuwa Kosovo ni nchi huru na ya kidemokrasi."

Kosovo Taifa dogo kabisa katika Balkan ,ilijitenga na Jamhuri ya Serbia mwaka jana 2008,miaka 9 tangu kumalizika vile vita vya kati ya 1998-1999 kati ya majeshi ya Serbia na wapiganaji wa kialbania wa kosovo.

Rais wa kosovo, Sejdiu amesema, " Hamasa za vita vile pamoja na chuki zilizoambatana navyo ziko bado katika vichwa n a taasisi za Serbia."

Akaongeza rais wa Kosovo kwamba, sera hizo za machafuko zinazofuatwa na Belgrade haziwsaidii waserbia wala eneo la balkan.

Wabunge 80 kutoka bunge la waakilishi 250 wa Serbia pamoja na kiongozi wa kila kundi la vyama vinavyowakilishwa Bungenib walitangaza leo watakuwa na kikao katika eneo la waserbia la Kosovo katika mji wa Mitrovica-mji uliogawika kati ya wakazi wa kiserbia na kialbania.

Machafuko ya kikabila yaliripuka huko hapo desemba na ja nuari na polsi imeongeza ulinzi katika mji huo.

babara za mji wa Pristina zilifungwa huku maalfu ya watu wsakijiandaa kw asherehe za leo n a baadhi ya mikahawa imejitolea pombe ya bure.

Kwa upande mwengine, Serbia na mshirika wake mkubwa Urusi,zingali zikipinga uhuru wa Kosovo ingawa uhuru huo umetambuliwa na Marekani pamoja na washirika wake barani ulaya.

Jana, rais Boric Tadic wa Serbia aliliambia shirika la habari la reutzers kwamba nchi yake kamwe haitaitambua Kosovo kama nchi huru.

Baraza kuu la UM limeidhinisha ombi la Serbia la kuitaka Mahkama Kuu ya kimataifa kuchunguza iwapo tangazo la uhuru la kosovo ni halali au la.

Uchunguzi huo utadumu kati ya mwaka mmoja hadi miwili.

Vita kati ya kosovo na Serbia vilimalizika 1999 kufuatia hujuma kali ya mabomu ya vikosi vya shirika la ulinzi la NATO yalivifanya vikosi vya Serbia kuuhama mkoa huo wa kusini mwake.Miaka iliofuatia ,Kosovo ikageuka eneo lililolindwa kimataifa na kusimamiwa na vikosi vya NATO vya kuhifadhi amani.