1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwaka tangu Msukosuko wa mabenki

15 Septemba 2009

Darasa gani limepatikana ?

https://p.dw.com/p/Jgxq
Angela Merkel na Frank-Walter SteinmeierPicha: AP

Maoni ya wahariri wa magazeti ya Ujerumani, yamechambua mada mbali mbali za ndani ya nchi-kuanzia kuuwawa kwa raia aliejitolea kusaidia raia mwengine hadi mjadala wa TV kati ya watetezi 2 wakuu wa wadhifa wa ukanzela:Bibi Angela Merkel wa chama cha CDU na waziri wa nje Walter Steinmeier.Hata mwaka tangu kuanza msukosuko wa sasa wa fedha, ni mada iliochambuliwa na wahariri hii leo.Ramadhan Ali aliewakagulia safu hizo za wahariri anaanza na msukosuko wa fedha .gazeti la NORDWEST-ZEITUNG laandika:

"Ni mwaka sasa tangu pale kufilisika kwa Lehman-Bank kutikisa hali ya uchumi ulimwenguni kote.Na sasa tena mabenki makubwa yanajipatia faida nono na kuwatunza mameneja wake vitita vikubwa vya fedha.Baada ya msukosuko unafuata msukosuko mwengine mtu aweza kudai hivyo.Hatahivyo, hakuna sababu ya kuchora sura mbaya.

Kwani, kimsingi, ushirikiano wa kimataifa kukabiliana na msukosuko huo umefanya kazi na hatua za kuukoa uchumi zilizochukuliwa na jamii ya kimataifa zimezaa matunda yake. Athari mbaya kama zile zilizotokana na msukosuko kama huo wa miaka ya 1930 zimeweza kuepukwa.Hiyo lakini, isiongoze kuzifumbia macho sababu za balaa hilo-nazo ni uroho wa fedha wa baadhi ya vigogo vya banki."

Ama gazeti la "NEUE PRESSE" linahisi wimbi la mstuko wa kufilisika kwa mabenki limesababisha hasara kubwa sana isiosemeka.Mabilioni ya dala pamoja na nafasi za kazi milioni kadhaa yameteketea. Neue Presse laongeza kusema:

"Nchini Ujerumani , ule mradi wa kulipwa fidia ya kitita cha fedha ili uachane na gari lako la zamani na ununue jipya na kule kupotezwa nafasi za kazi kiasi fulani kuna hadaa.Kwani, hatima mbaya ya viwanda vya magari na kupunguzwa wafanyakazi viwandani kutafuata.Wanabenki tayari wameshafungua Casino zao kucheza tena kamari. Wmeshaanza biashara yao na wanafurahia malipo yao manono.

ambo moja ni hakika, hata msukosuko huu ukimalizika,mwengine utakuja tu."

Gazeti la NEUE TAG linauchambua ule mjadala wa TV kati ya watetezi 2 wanaoania wadhifa wa ukanze katika uchaguzi wa mwishoni mwa mwezi huu nchini Ujerumani: Bibi Angela Merkel na Bw. Walter Steinmier.Gazeti laandika:

"Hata ikiwa katika mjadala ule hakuna alieibuka mshindi wazi,walioshindwa ni watangazaji 4 wa TV waliouendesha.Kutokana na maswali yao ,uliweza kuwahurumia Bibi Angela Merkel na Bw.Steinmeier.Mara nyingi yalikuwa maswali ya kipumbavu....Badala ya kuegemea zaidi tofauti za mawazo ya kisiasa kati ya watetezi hao 2 -Knzela na mpinzani wake, gengi hilo la watangazaji 4,likisaka mmoja wao ateleze ulimi tu.."

Gazeti la LEIPZIGER VOLKSZEITUNG linauliza:

Nani alifaidika na mjadala ule ? Labda lajibu gazeti, ni Bw.Steinmeier kwavile,hakujitoa vibaya kuliko katika kampeni zake za hadi sasa na ndio maana alitamba na kuwasangaza wengi.Kanzela Merkel ambae kiusomi ni bora zaidi, alifanya kosa la kukunja uso wakati akizungumza na kufanya maswali yote aliotupiwa kuonekana kama adha tu kwake.Alipogundua kosa hilo, alibadili mtindo na kuanza kutabasamu.Bw. Steinmeier kwa upande wake, alibainisha ana umahiri wa kuwa kanzela......"

Mtayarishi: Ramadhan Ali /DPA

Mhariri: M.Abdulrahman