1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwalimu wa Uingereza ahukumiwa kifungo cha siku 15

30 Novemba 2007
https://p.dw.com/p/CUwr

Mahkama nchini Sudan imemuona mwalimu wa Uingereza kuwa na hatia ya kuwatukana Waislamu kwa kuliruhusu darasa lake kumwita dubu wa kuchezea jina la Muhammad ambalo ni jina la mtume wa Waislamu.

Gillian Gibbons amehukumiwa kifungo cha siku kumi na tano gerezani na baadae atarudishwa kwao Uingereza. Mjini London waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Miliband amesema amevunjwa moyo sana na hukumu hiyo na amemwita balozi wa Sudan nchini humo kwa ajili ya kutowa ufafanuzi.

Gibbons ameepuka kushtakiwa kuchochea chuki na kuonyesha dharao kwa imani za dini.

Mmojawapo wa mawakili wanaomtetea amesema atakata rufaa kupinga hukumu hiyo.