1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanahiti: zawadi ya unyago Uzaramoni

16 Mei 2012

Mwanahiti ni sanaa ya kuchongwa ambayo anapewa binti mwanamwali unyagoni katika kabila la Wazaramo na baadhi ya makabila mengine ya Pwani ya Tanzania.

https://p.dw.com/p/14wN2
sanamu za wanyama
Sanamu za wanyamaPicha: AP

Uvaliwa shingoni na kuwekwa mchagoni. Wazaramo wanaamini kuwa Mwanahiti ana uwezo wa kumlinda binti mwanamwali wakati wa unyago na katika maisha ya ndoa. Huchongwa kutoka mti wa Mkongo, ambao ni mti mgumu sana hauwezi kuliwa na wadudu huku akiwekewa nakshi kadhaa kuweza kuonekana katika hali ya kutisha kwa yule anayemtazama.

Mwandishi: Adeladius Makwega

Mhariri: Miraji Othman

Makala: Utamaduni na Sanaa