1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanajeshi wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia azungumza

1 Septemba 2009

Siku kama leo, tarehe Mosi Septemba, mwaka 1939, miaka 70 iliopita, manuwari ya Kijerumani, iliishambulia kambi ya kijeshi ya Ngome ya Westerplatte, katika bandari ya Danzig, hivi sasa bandari hiyo inaitwa Gdansk.

https://p.dw.com/p/JNDF
Wakuu wa Ulaya wakiweka mishumaa kwenye Kumbukumbu ya Vita Vikuu vya pili vya Dunia huko Gdansk,Poland.Picha: AP

Hiyo ndio ilikuwa operesheni ya kwanza ya kijeshi katika Vita Vikuu vya Pili vya Dunia. Wakati huo huo, vikosi 62 vya jeshi la Ujerumani, vikisaidiwa na ndege 1,300, vilianza kuivamia Poland. Vita hivyo vilitapakaa katika sehemu mbali mbali za dunia, na medani za vita pia zilitanda huko Afrika na Asia, ambako washirika wa Ujerumani -Wajapani na Wataliana- walipambana pia na majeshi ya Waafrika kutoka makoloni ya Muengereza, kama vile yale ya Afrika Mashariki. Mmoja aliyeshiriki katika vita Vikuu vya Pili vya Dunia ni Ali Sykes kutoka Tanganyika ambaye alipelekwa Burma kuyasaidia majeshi ya Kiengereza yaliokuwa yanapambana na Wajapani. Othman Miraji Na Bw Ali Sykes.

Mahojiano/Othman Miraji/Ali Sykes