1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamfalme Harry na Markle wafunga ndoa

Saumu Mwasimba
19 Mei 2018

Harusi ya Mwanamfalme wa Uingereza Harry na mpenzi wake Meghan Markle yafana mjini London ikiwa imehudhuriwa na wageni 600 walioalikwa na kutazamwa na maelfu nchini humo na nje ya Uingereza

https://p.dw.com/p/2y0GE
UK | Hochzeit Prinz Harry & Meghan Markle | Brautpaar vor der Kirche
Picha: Reuters

Mwanamfalme Harry amemuoa  Meghan Markle  katika  sherehe kubwa leo Jumamosi  katika  kanisa  la  Kifalme la  Mtakatifu George  ndani  ya  kasri  la  Windsor. Mamilioni  ya  watazamaji katika  televisheni  duniani  kote wamefuatilia sherehe hiyo sambamba na  wageni  chungunzima mashuhuri walihudhuria.

Harry  alijumuika  na  kaka  yake  na ambaye  ni  msaidizi  wake wa  karibu  katika  harusi  hiyo, mwanamfalme William , mwenye umri  wa  miaka  35, wakati mama yake Markle mwenye  umri  wa miaka  62, Doria Ragland, akiongozana  nae.  Markle alivalia shela jeupe lililotengenezwa na kampuni ya kifaransa iliyoko London ya Givenchy. Kofia zilitawala sherehe hiyo huku mama harusi Doria Ragland akiwa amevalia suti ya rangi ya kijani na kutupia kofia yake. Wageni pia wakiwemo Oprah Winfrey na Stella McCatney walitupia kofia za rangi ya pinki zilizorandana vizuri na nguo walizovalia.Ndoa hiyo ilifungishwa na kiongozi mkuu wa kanisa la Anglikana la Uingereza askofu mkuu wa Canterburry Justin Welby.

UK | Hochzeit Prinz Harry & Meghan Markle | Herzogin Catherine/Kate
Picha: picture-alliance/dpa/PA Wire/J. Brady

Harusi hiyo inatajwa kwamba ilikuwa ya mvuto wa kipkee ya kifalme ikilinganishwa na ya Kate Middleton aliyeolewa na mwanamlfame William mwaka 2011 ambapo aliyeangaziwa zaidi kwenye harusi hiyo alikuwa dada wa Kate Middleton Pippa Middleton.

Viongozi mbali mbali duniani wametuma pongezi kwa wanandoa hao wapya katika ufalme wa Uingereza akiwemo waziri mkuu wa Canad Justin Treudeu. Miongoni mwa wageni 600 waalikwa ni pamoja na waliowahi kuwa wapenzi wa Harry Cressida Bonas alivalia kigauni cha michoro cha rangi ya pinki kijani na njano huku mpenzi mwengine wa zamani wa Harry Chelsy Davy akitokea na kigauni kifupi cha rangi ya buluu ya kuiva au (Navy Blue)mradi kila aliyehudhuria harusi hiyo alipendeza kivyake.

UK | Hochzeit Prinz Harry & Meghan Markle |
Picha: Reuters/H. McKay

Tukio  hilo  la  harusi  lililochukua  muda  wa  saa  moja  lilifuatiwa na  msafara  wa  dakika  20  nje ya  kasri  katika  gari  la kukokotwa  na  farasi.

Baba  wa bi harusi hakuhudhuria  harusi  hiyo. Thomas Markle, mwenye  umri  wa  miaka  73, alifanyiwa  upasuaji wa  moyo  siku ya  Jumatano.

Harry   na  Markle  wamewakaribisha  mamia  ya  watu kushuhudia sherehe  hizo  katika  viwanja  vya  kasri  la  kifalme, wakati  mamia  kwa  maelfu  ya  watu  wanaosherehekea  harusi hiyo  wakijipanga  katika  njia  ilikopita  gari  ya  kukokotwa  na farasi.

UK | Hochzeit Prinz Harry & Meghan Markle | Brautpaar in Kutsche
Picha: Reuters/H. McKay

Polisi  imepiga  marufuku kurusha  maua  na  mapambo  wakati wa  msafara  huo , wakielezea  kuhusu  wasi  wasi  wa  usalama. Wageni waalikwa wanajumuika katika sherehe maalum ya kula na kunywa pamoja na Prince Harry na mkewe Markle  ambapo vyakula mbali mbali vimeandaliwa kwa ajili ya wageni hao.

Uingereza  imekuwa  ikivutia  dunia kwa harusi  za kifalme, matukio ya sherehe za kuvutia  na  haiba  ambayo  inasababisha   mvuto kwa  familia  ya  kifalme.

Mwandishi:  Saumu Mwasimba

Mhariri:Caro Robi