1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamfalme Harry wa Uingereza aondoka Afghanistan

1 Machi 2008
https://p.dw.com/p/DGEW

LONDON:

Mwanamfalme Harry wa Uingereza ameondoka Afghanistan baada ya vyombo vya habari kufichua kuwa yupo nchini humo pamoja na kikosi cha Uingereza kupigana dhidi ya Wataliban.Wizara ya Ulinzi ya Uingereza imesema,usalama wa Mwanamfalme Harry umehatarishwa baada ya habari hiyo kuripotiwa na vyombo vya habari vya kimataifa.

Mwanamfalme huyo alikuwepo katika Wilaya ya Helmand kusini mwa Afghanistan kwa takriban majuma kumi akipigana katika mstari wa mbele dhidi ya Wataliban.Hapo awali ilitazamiwa kuwa Mwanamflame Harry alie na umri wa miaka 23 atabakia Afghanistan kwa muda wa miezi minne.