1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanamke auawa kwa bomu la kifurushi Ufaransa

7 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/CYYR

PARIS.Mwanamke mmoja amekufa na mtu mwengine amejeruhiwa baada ya kufungua kifurushi kilichokuwa na bomu huko Ufaransa.

Kifurushi hicho kilitumwa kwenye ofisi ya uwakili jijini Paris ambapo katibu mukhtasi wa kampuni hiyo alipokifungua alilipukiwa na bomu lililokuwa ndani.

Wakili ambaye kivurushi hicho kilitumwa kwake alijeruhiwa vibaya na bomu hilo la kutengenezwa kienyeji.

Ofisi za kampuni hiyo ziko katika jengo moja na ofisi za kampuni ya zamani ya uwakili ya Rais Nicolaus Sackozy.Hakuna kikundi chochote kilichodai kuhusika na shambulizi hilo.