1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Kuuawa kwa Mmisri.

Abdu Said Mtullya9 Julai 2009

Mwanamke mmoja wa kimisri aliuawa kwa kupigwa visu kwenye mahakama ya mjini Dresden, mashariki mwa Ujerumani.

https://p.dw.com/p/IkOU

Mwanamke mmoja wa kimisri aliuawa kwa kupigwa visu kwenye mahakama ya mjini Dresden, mashariki mwa Ujerumani.

Mwanamke huyo, Marwa El Sherbin, alishambuliwa na Mjerumani mwenye asili ya Urusi jumatano iliyopita.

Mama huyo aliuawa kwa sababu ya kumfikisha mahakamani Mjerumani huyo.

Mwaka jana mama huyo alikuwa kwenye uwanja wa michezo katika mji wa Dresden ambako palikuwa na mabishano juu ya vitu vya kuchezea kwa ajili ya watoto.

Katika purukushani zilizotokea, kijana wa Kirusi mwenye asili ya kijerumani alimkashifu mama huyo wa Kimisri kwa kumwita kahaba na gaidi.

Mwanamke huyo, Marwa El Sherbin, aliekuwa mjazito alimshtaki mahakamani kijana huyo wa kijerumani na kutokana na hayo kijana huyo alimshambulia Mmisri huyo kumchoma visu mara 18.

Marwa, aliekuwa a na mtoto mmoja, alijeruhiwa vibaya na alifariki baadae. Mwili wa hayati ulirudishwa nchini Misri na kuzikwaa jumatatu iliyopita katika mji wa Alexandria.

Kifo cha mama huyo kinazungumziwa katika vyombo vyote vya habari nchini Misri.

Licha ya balozi wa Ujerumani nchini Misri Bernd Erbel, kulaani mauaji hayo, watu nchini Misri wamekuja juu.

Balozi huyo amesema anataraji adhabu kali kwaa mmuaji na kwamba hayo yanashughulikiwa na mahakama ya Ujerumani.

Balozi Erbel amesema anatumai kuwa alietenda uhalifu huo ataadhibiwa vikali.

Aidha aliongeza kuwa aliemwuua mwanamke huyo wa Kimisrri hawakilishi umma wa Ujerumani ambao kwa sasa unashikamana na kuwathamini watu wa Misri.

Mwuuaji huyo alitenda uhalifu huo kutokana na uamuzi wake peke yake.

Hata hivyo muhalifu huyo kwa sasa amekamatwa kwa tuhuma za mauaji.Uchunguzi unafanyika kwa uthabiti wote.

Wanasiasa hadi wa ngazi za juu sasa pia wanaushughulikia mkasa huo wa kusikitisha.

Kansela wa Ujerumani, anaehuhduria mkutano wa nchi tajiri, G 8, katika mji wa Laquilla nchinin Italia, anakusuduia kukutana na rais Hosni Mubarak wa Misri ili kuzungumzia mkasa huo.

Rais Mubarak pia anahudhuria mkutano wa mjini Laquilla. Watakutana mwanzoni mwa mazungumzo ya G 8.

Wakati huo huo, watu nchini Misri wanaamini kwamba kuuawa kwa Mmisri mwenzao nchini Ujerumani kutafunikwa.

Katika kituo kimoja cha radio nchini Misri, magazeti ya Ujerumni yamekakaririwa yakisema kuwa alietenda uhalifu huo ni mwendawazimu tu.

Lakini gazeti moja linalohusiana na gazeti maaruf la al-ahram limesema katika safu yake ya maoni kuwa mauaji hayo ni kitendo cha chuki dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Kijana mmoja nchini Misri akizungumza kwenye televisheni ameuliza "Inakuaje mwanamke wa Kiislamu anaitwa gaidi ati kwa sababu ya kuvaa hijabu.Mnazungumzia juu ya uhuru, jee uhuru wetu sisi uko wapi? Sisi siyo magaidi na wala hatutakuwa magaidi.Tutavaa nguo jinsi tunavyotaka na tukwenda tunakotaka"

Mtangtazaji wa televisheni ya Al Qahira al Youm amewataka wasikilizaji na watazamaji wapeleke barrua pepe kwa bolozi wa Ujerumani nchini ili kuonyesha jinsi watu wa Misri walivyoghadhibika kutokana na kuuawa kwa mama huyo wa kimisri.

Mwandishi/Jürgen Stryjak/Mtullya,Abdu

Mhariri: Miraji Othman