1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanandondi Tyson apigwa marufuku kuingia Uingereza

16 Desemba 2013

Bingwa zamani wa uzito wa juu duniani Mike Tyson amepigwa marufuku kuingia nchini Uingereza kuzindua kitabu chake. Hatua hiyo inatokana na mabadiko katika sheria za uhamiaji.

https://p.dw.com/p/1AZct
Mike Tyson
Picha: picture-alliance/dpa

Vyombo vya habari nchini humo viliripoti kwamba bondia huyo wa Marekani ambaye aliwahi kuhukumiwa kwa ubakaji akitazamiwa kuwasili nchini humo wiki hii akitokea paris-Ufaransa, kwa uzinduzi wa kitabu cha maisha yake, kiitwacho “ ukweli usipingika.” Sheria mpya za uhamiaji hata hivyo zinaeleza kwamba mtu yeyote aliyewahi kupatikana na hatia na kutumikia kifungo cha zaidi ya miaka mine jela hatoruhusiwa kuingia Uingereza .

Tyson mwenye umri wa miaka 47 alihukumiwa kifungo cha miaka sita mwaka 1992 kwa kumbaka mrembo mmoja wa zamani. Mchapishaji wa kitabu chake harper Collins alikaririwa akisema kulikuwa na mabadiliko katika sheria za uhamiaji uza Uingereza Desemba mwaka jana 2012 ambazo hawakuzijuwa na kutokana na hayo walilazimika kubadili ratiba na badala yake kitabu hicho kuzinduliwa eneo moja la jiji la Paris.

Tyson alikuwa bingwa wa kwanza wa dunia mwenye umri mdogo 1986 alipokuwa na miaka 20 na bondia wa kwanza kushikilia mataji matatu makubwa ya ubingwa wa ndondi duniani kwa wakati mmoja mwaka mmoja baadae. Mwaka 2000 Tyson alipigana nchini Uingereza dhidi ya Julius Francis mjini Manchester na baadae mwaka huo huo akachuana baadaye na Lou Savarese mjini Glasgow.

Mwandishi: Mohammed Abdul-Rahman

Mhariri: Mohammed Khelef