1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwandishi habari aachwa huru.

25 Desemba 2007
https://p.dw.com/p/Cfzb

Mogadishu. Watu wenye silaha nchini Somalia wamemwacha huru mwandishi habari raia wa Ufaransa ambaye alitekwa nyara siku nane zilizopita katika jimbo la kaskazini la Puntland. Afisa wa serikali amesema kuwa Gwen Le Gouil, ambaye alikuwa akifanyakazi ya kurekodi kipindi maalum cha televisheni kuhusiana na wakimbizi , aliachiwa huru bila masharti. Wateka nyara hao walidai hapo mapema kiasi cha dola za Marekani 80,000. Wakati huo huo Burundi imepeleka nchini humo kundi la pili la wanajeshi wapatao 90 wa kulinda amani katika mji wa Mogadishu na kuongeza katika idadi ya wanajeshi 100 ambao wamewasili siku moja kabla.

Wanajeshi hao ni sehemu ya awamu ya kwanza ya msaada ambao umecheleweshwa mno kwa wanajeshi 1,600 kutoka Uganda ambao waliwasili nchini humo March mwaka huu ikiwa ni sehemu ya jeshi la umoja wa Afrika lenye wanajeshi 8,000 wa kulinda amani nchini humo.