1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Mwanzo mpya nchini Cote I'voire baada ya Gbagbo kukamatwa

Abdu Said Mtullya12 Aprili 2011

Laurent Gbagbo sasa yupo chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa

https://p.dw.com/p/10rgR
Aliekuwa Rais wa Cote I'voire Laurent Gbagbo, sasa amekamatwaPicha: dapd

Aliekuwa anang'ang'ania madaraka ya Urais nchini Cote Ivoire Laurent Gbabgo amejisalimisha baada ya makao yake kushambuliwa na majeshi ya Ufaransa, na ya Alassane Ouattara ,anaetambuliwa na jumuiya kimataifa kuwa Rais wa Cote Ivoire.

Gbagbo sasa amewekwa chini ya ulinzi wa Umoja wa Mataifa.Gbagbo alikamatwa ndani ya handaki ambamo alikuwa amejificha. Mwanasiasa huyo alikataa kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi wa Urais uliofanyika mwezi desemba mwaka jana nchini Cote Ivoire.

Muda mfupi baada ya Gbagbo kukamatwa, Ouattara anaetambuliwa kuwa Rais alisema kuwa aliamrisha uchunguzi juu ya matendo ya Gbagbo.Ouattara amesema Gbagbo, mkewe na washirika wake watafanyiwa uchunguzi na idara za sheria.Ouattara pia ametoa mwito wa kuleta maridhiano nchini.

Juu ya kukamatwa kwa Gbagbo ,waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Guido Westerwelle amesema ,anatumia kuwa vita vya wenyewe kwa wenyewe sasa vitamalizika nchini Cote Ivoire na kwamba patakuwa na mwanzo mpya wa kidemokrasia.